Ndege SJ182 ilikuwa inaelekea Pontianak katika kisiwa cha Borneo. Zaidi ya watu 50 walikuwa wakisafiri katika ndege hiyo, maafisa wamesema.
Kitengo cha kufuatilia ndege, Flightradar24, kimesema Boeing 737 “ilirudi chini kutoka anga za juu kwa zaidi ya futi 10,000 katika muda wa chini ya dakika moja, takriban dakika 4 baada ya kuruka kutoka Jakarta.”
“Ndege hiyo iliyopotea hivi sasa inatafutwa na kwa uratibu wa Shirika la Taifa la Kutatufa na Uokoaji ikishirikiana na Kamati ya Taifa ya Usalama wa Usafiri,” msemaji wa serikali Adita Irawati amesema katika taarifa yake.