Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:08

Mswaada wa Bunduki: Maseneta Warepublikan na Wademokrat waelekea kukubaliana


Aina ya bunduki za kivita zinazomilikwa kiholela na baadhi ya watu nchini Marekani.
Aina ya bunduki za kivita zinazomilikwa kiholela na baadhi ya watu nchini Marekani.

Maseneta wa Marekani wameelekea katika  makubaliano ya pande mbili kuhusu mswaada wa udhibiti wa ghasia za bunduki , msemaji mkuu wa Wademocrat alisema Jumanne.

Amesema pia kuna uwezekano wa kupiga kura wiki hii juu ya mpango huo ambao ni majibu ya bunge kuhusu ufyatuaji risasi uliofanyika texas na New York uliolitikisa taifa.

Siku tisa baada ya wapatanishi wa Seneti kukubaliana na pendekezo la mfumo na miaka 29 baada ya bunge kupitisha mara ya mwisho hatua kuu ya kuzuiya silaha , Seneta Chris Murphy ,Mdemocratik- Connecticut aliwaambia waandishi wa habari kwamba makubaliano ya mwisho kuhusu maelezo ya pendekezo hilo yanakaribia.

Pendekezo ambalo wabunge wamekuwa wakilifanyia kazi litaongeza ukaguzi zaidi kwa vijana wanaonunua silaha na kuongeza adhabu zaidi kwa walanguzi wa bunduki.

Pia ingetoa pesa kwa majimbo na jumuiya zinazolenga kuboresha usalama wa shule na mipango ya afya ya akili.
Seneta Murphy wa Connecticut alisema: “Naamini kwamba wiki hii tutapitisha sheria ambayo itakuwa muhimu katika kudhibiti ghasia za bunduki , ambayo bunge litakuwa limepitisha kwa miaka 30. Haya ni mafanikio.

Lililo muhimu zaidi ni mafanikio ya pande mbili, na nina furahi kuungana na rafiki yangu, seneta Cornyn kuzungumiz machache kuhusu kifungu cha sheria ambacho wenzetu wataweza kuangalia kwa matumaini katika muda mfupi.”

XS
SM
MD
LG