Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:25

Mkuu wa misaada wa UN atahadharisha janga la njaa Tigray


UN yatahadharisha kutokea janga la njaa Tigray
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:53 0:00

UN yatahadharisha kutokea janga la njaa Tigray

Mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths, amesema Jumanne huenda kuna njaa katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia.

Anaeleza eneo hilo kwa miezi kadhaa kumekuwepo na uzuiaji wa fursa za kupeleka misaada na imepelekwa asilimia 10 ya kile kilichohitajika katika eneo hilo lenye vita.

Griffiths aliliambia shirika la habari la Reuters katika mahojiano kuwa ombi lake lilikuwa rahisi: “Ruhusuni hayo malori yapeleke misaada”.

Tatizo hili limekuzwa kibinadamu, linaweza kurekebishwa kwa serikali ya Ethiopia kuchukua hatua, alisema.

Abiy Ahmed
Abiy Ahmed

Vita viliibuka miezi 10 iliyopita kati ya wanajeshi wa serikali na vikosi vitiifu vya Tigray People’s Liberation Front (TPLF), ambavyo vinadhibiti Tigray.

Maelfu wamekufa na zaidi ya watu milioni mbili wamelazimika kuhama nyumba zao.

Tulibashiri kwamba kulikuwa na watu laki nne waliopo katika hali kama ya njaa, na dhana ilikuwa kwamba ikiwa hakuna msaada wa kutosha utakaowapa wangeingia katika janga la njaa, alisema Griffiths, akimaanisha tathmini ya Umoja wa Mataifa ya mwezi Juni.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la Reuters

CN:

XS
SM
MD
LG