Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:05

Mkuu wa masuala ya nyuklia wa UN kuzuru Tehran


Rafael Mariano Grossi
Rafael Mariano Grossi

Mkuu wa kituo kinachofuatilia masuala ya nyuklia cha Umoja wa Mataifa, Rafael Grossi, atasafiri kwenda Tehran wikiendi hii kwa mazungumzo, ambayo yanaweza kupunguza mivutano kati ya Iran na mataifa ya magharibi wanadiplomasia walisema hayo Jumamosi.

Wameeleza hatari imekuwa ikiongezeka na kudumaza mazungumzo juu ya kufufua tena makubaliano ya nyuklia ya Iran.

Wanadiplomasia watatu ambao hufuatilia kwa karibu idara ya nishati ya Atomic (IAEA), walisema safari ya Grossi kabla ya mkutano wa wiki ijayo, wa bodi ya magavana wa mataifa 35 ya IAEA, ilithibitishwa.

Wawili walisema Grossi alitakiwa kuwasili Tehran, mapema Jumapili na kukutana na mkuu mpya wa idara ya nishati ya Atomic ya Iran, Mohammad Eslami.

IAEA ilizijulisha nchi wanachama wiki hii, kwamba hakuna maendeleo juu ya maswala mawili makuu, moja likiwa kuelezea kuhusu uranium iliyogundulika katika maeneo kadhaa ya zamani.

Jambo la pili ni suala la maeneo ambayo hayajatangazwa na kupatiwa fursa ya haraka kufuatilia baadhi ya vifaa, ili idara iweze kuendelea kufuatilia sehemu za mpango wa nyuklia wa Iran, kama ilivyotolewa kwenye makubaliano ya mwaka 2015.

XS
SM
MD
LG