Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:35

Mkutano wa SADC wahamasisha ukuaji uchumi, kilimo na madini


Rais Félix Tshisekediya wa DRC akikabidhiwa uenyekiti wa SADC na Rais wa Malawi Lazarus Chakwera, Kinshasa, RDC, August 17 2022.
Rais Félix Tshisekediya wa DRC akikabidhiwa uenyekiti wa SADC na Rais wa Malawi Lazarus Chakwera, Kinshasa, RDC, August 17 2022.

Mkutano wa 42 wa viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC,  Alhamisi umemazilika huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika mji mkuu wa Kinshasa. 

Mkutano wa mwaka huu ulikuwa na ujumbe “ kuhamasisha viwanda kupitia, usindikaji wa kilimo, faida ya madini, na mifumo ya thamani ya kikanda kwa kujumuisha wote na ukuaji stahmilivu.”

Masuala makuu katika kikao hicho ilijumuisha uzinduzi wa jopo la wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali waliohudhuria, wakifatuiwa na utoaji wa medali kuwakumbuka na kuwapa heshima waanzilishi wa SADC.

Katika kuingiza enzi mpya ya uongozi wa SADC, sherehe za ufunguzi pia zilishuhudiwa na kukabidhi uenyekiti wa SADC kutoka kwa jamhuri ya Malawi na kijiti kukamatwa hivi sasa na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Hii ilifuatiwa na taarifa ya kukubali iliyotolewa na mwenyekiti mpya wa taasisi hiyo Rais Felix Tshisekedi wa DRC na mwenyeji wamkutano wa 42 wa SADC.

Rais Tshisekedi anaeleza: "Nitahakikisha natekeleza program za kuendeleza miundo mbinu na huduma katika ukanda ambalo linahusika moja kwa moja na mikakati yetu mikuu katika kuchochea muingiliano wa kiuchumi na kutokomeza umaskini katika ukanda wa SADC.”

Mkutano huu umekuja wakati ambapo nchi mwenyejiti inakabiliwa ghasia mpya upande wa Mashariki. Mbele ya viongozi wenzake, Rais Felix Tshisekedi alishutuma vikali ‘ uhuni na ukatili unaofanywa dhidi ya nchi ya jirani yake Rwanda.

Baadhi ya mataifa wanachama wa SADC kama vile Malawi na Tanzania wanachangia wanajeshi katika kikosi maalum cha ulinzi wa amani cha Umoja wa Mataifa MONUSCO.

Rais wa DRC ameongeza kuwa:“ Kwa Jamhuri ya Afrika Kusini, jamhuri ya Malawi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wametoa wanajeshi wao kwa gharama kubwa ya amani upande wa mashariki mwa nchi yetu.”

Mwanachama mwingine wa umoja huo, Msumbiji pia inakabiliana na uasi wa wanamgambo katika majimbo ya kaskazini. Jeshi la kikanda linalojulikana kama SAMIM, pamoja na majeshi kutoka Rwanda wamefanikiwa kuwasukuma kutoka katika eneo hilo waasi wanaohusishwa na Islamic State.

Rais wa Malawi Lazarus chakwera amesisitiza waoz wa Afrika kutafutua masuluhisho yake wenyewe.

//Rais Lazarus Chakweera, Malawi//

“Hakuna suluhisho hata moja kutoka nje ya Afrika ambalo linakuja kuijenga Afrika kwa jinsi sisi tunavyotaka. Siyo wamarekani, siyo wa Ulaya, siyo wa Asia. Huenda wanaweza kutupa wazo la hapa na pale, na maelezo moja au mawili, dola milioni chache ambazo hazifanyi z chochote katika mifuko yetu ukilinganisha na kiwango ambacho wanachowapa wa magharibi au wa mashariki.”

//Rais Lazarus Chakweera, Malawi//

“Vurugu ambayo tumewaruhusu magharibi kuifanya nchini DRC ni dhambi lazima tutubu, na tuache na kukataakurejewa tena kwa jambo hilo kwingineko kokote katika eneo letu. Kwahiyo tuwaonyeshena kuwaambia tuonyeshe na kuieleza dunia kwa sauti moja kwamba Afrika iko wazi kwa biashara, lakini Afrika haiuzwi.”

Mkutano pia uitathmini maendeleo ya muingiliano wa kikanda kulingana na utashi wa SADC kama ulivyoelezewa katika RISDP 2020 mpaka 2030 na Vision 2050 ambapo suala la amani, kujumuisha wote, suhindani, eneo hilolenye viwanda kati ya kipato cha kati na cha juu ambako raia wote wanafurahia mafnaikio endelevu ya kiuchumi, sheria, na uhuru.

Khadija Riyami VOA Washington

XS
SM
MD
LG