Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:10

SADC yataka Zimbabwe iondolewe vikwazo vyote bila masharti


Rais wa Malawi Lazarus Chakwera akitoa hotuba ya kukubali uteuzi kama mwenyekiti wa SADC. Lilongwe, Malawi, on Aug. 17, 2021.
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera akitoa hotuba ya kukubali uteuzi kama mwenyekiti wa SADC. Lilongwe, Malawi, on Aug. 17, 2021.

Jumuiya ya SADC imetoa wito wa kuondolewa haraka na bila masharti vikwazo dhidi ya serikali ya Zimbabwe.

Taarifa iliyotolewa na rais wa Malawi Lazarus Chakwera ambaye ni mwenyekiti wa SADC yenye mataifa wanachama 16 wa nchi za kusini mwa Afrika imesema ingependa kuona hatua hiyo ikichukuliwa kwa haraka.

“Sisi kama SADC tuna wasiwasi kuhusu vikwazo vinavyoendelea kwa watu binafsi na makampuni nchini Zimbabwe," alisema Chakwera.

Rais huyo alisema vikwazo hivyo vya muda mrefu vimeizuiya Zimbabwe kuboresha uchumi wake, usalama wa binadamu na ukuaji endelevu.

Zimbabwe imekuwa chini ya vikwazo vya kiuchumi kutoka Marekani na Jumuiya ya ulaya EU, vikilenga watu maalumu na makampuni, jambo ambalo serikali inalaumu kuwa ni sababu ya matatizo ya kiuchumi nchini humo.

Taarifa ya SADC imesema Zimbabwe na SADC waliweka nia ya dhati kuzungumza na wadau wakuu kuhusu kuimarisha demokrasia, utawala ha haki za binadamu.

XS
SM
MD
LG