Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:01

Mkutano wa rasilmali za majini wafikia makubaliano


Mkutano wa rasilmali za majini wafikia makubaliano
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:05 0:00

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akihutubia Mkutano wa rasilmali za majini

Mkutano wa siku tatu wa kuendeleza na kustawisha uchumi endelevu ya rasilimali za majini nchini Kenya umefikia tamati Jumatano, huku viongozi wa mataifa mbalimbali wakiwemo wajumbe kutoka zaidi ya nchi 183 wakifikia makubaliano katika nyanja mbalimbali.

Viongozi na wajumbe mbalimbali waliohudhuria mkutano huo Nairobi, wamekubaliana kuimarisha uongozi wa kisiasa na ushirikiano wa kimataifa kupitia matumizi ya data na habari za kijasusi kudhibiti tishio la uharamia kuhusu rasilimali za maji.

Kando na kuweka ahadi za kifedha kustawisha uchumi utokanao na rasilimali za majini, makubaliano yamewekwa ya kujenga uwezo katika nchi masikini, kuendesha ufanisi zaidi kwenye mito, maziwa na bahari.

Pia kutumia rasilimali za sayansi na teknolojia kwa ajili ya nchi hizi na vile vile kudumisha usalama katika vyanzo mbalimbali vya maji pamoja na kuhamasisha ufuatiliaji na uhifadhi wa vyanzo hivyo.

Kama kiashiria cha kuonyesha vitendo halisi, wajumbe wameafikiana kuanzisha viwango tofauti vya kutunza mazingira, kuimarisha mipango na kusaidia nchi masikini kupona kutokana na majanga yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi na vile vile kuhakikisha upo ubora halisi wa uvuvi halali.

Serikali ya Kenya, Japan, Canada ziliandaa mkutano huo kwa ubia na kufadhiliwa na mataifa kama vile Norway, Qatar, Uingereza, Umoja wa Ulaya, Uchina, Ureno, Nigeria, Ufaransa, Afrika Kusini miongoni mwa matifa mengine pamoja na mashirika ya kimataifa.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennedy Wandera, Kenya.

XS
SM
MD
LG