Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:11

Katibu Mkuu wa UN amteua Mtanzania kuwa kaimu Mkurugenzii wa UNEP


Katibu Mkuu Antonio Guterres
Katibu Mkuu Antonio Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Joyce Msuya raia wa Tanzania kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji MKuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Mazingira, UNEP.

Vyanzo vya habari vimemnukuu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric akisema Katibu Mkuu amechukua hatua hiyo huku akiendelea kumtafuta atakaye chukua nafasi hiyo ya UNEP.

Msuya amekuwa akitumikia nafasi ya Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Mazingira lenye makao yake Nairobi, Kenya.

Nafasi hiyo ilikuwa iko wazi baada ya kujiuzulu kwa Erik Solheim, anayekabiliwa na kashfa za matumizi ya fedha katika safari yake.

Ripoti ya ukaguzi wa fedha ambayo ilichapishwa na gazeti la Uingereza la The Guardian, inaonyesha Solheim alitumia jumla ya $488,518 (£382,111) akisafiri siku 529 kati ya siku 668.

Alikuwa hayupo afisini kwa takriban asilimia 80 ya muda wake kazini.

Ripoti hiyo inasema gharama hiyo imetia doa sifa za UN kama shirika ambalo husimamia mashauri endelevu ya ulinzi wa mazingira.

Msuya, mwaka 2017 alikuwa ni Mshauri wa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Mashariki ya Asia na Eneo la Pacific jijini Washington, DC.

Pia anauzoefu wa muda usio pungua miaka 20 katika nyanja za maendeleo ya kimataifa ikiwemo biashara, mikakati, ajira, ujuzi wa utawala na ubia, na kutekeleza majukumu mbalimbali katika bara la Afrika, Marekani ya Kusini.

Msuya ana shahada ya Uzamili ya Sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, Canada na Digree ya Sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde, Scotland. Ameolewa na ana watoto wawili.

XS
SM
MD
LG