Huku hali ya usalama ikiendelea kuwa tete kufuatia shambulizi la bomu katika sinagogi na mauaji huko Ubelgiji na Ufaransa yaliyofanywa na washukiwa Waislam wenye msimamo mkali.
Maafisa kutoka nchi 27 za EU wameeleza wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya Wayahudi, kuhamasishwa kwa vijana kuchukua misimamo mikali katika mitandao, utumiaji wa ujumbe wa simu kupitia mfumo wa kuficha mawasiliano yawe baina ya watu wawili yanafanywa na wahalifu au watu wenye misimamo mikali, na umuhimu wa kuharakisha kuwaondoa wao ambao wanaweza kuwa ni hatari kwa umma.
Lakini wito kadhaa wa kuimarisha zaidi usalama kote Ulaya pia unaleta wasiwasi zaidi kwani suluhisho linalozungumziwa linaweza kukandamiza haki ya uhuru wa kusafiri na haki ya kukusanyika Ulaya.
Italia imeanzisha ukaguzi katika mipaka kuzuia uwezekano wa kuongezeka mvutano katika vita ya Israel na Hamas.
Pia hilo liko Denmark na Sweden, kwa sababu ya kile wanachosema ni “tishio la magaidi wenye misimamo mikali ya kiislam.”
Polisi wengi zaidi wameandaliwa huko Ubelgiji, Ufaransa na Ujerumani.
Mkuu wa sera ya kigeni ya EU Josep Borrell anaamini kuwa sehemu ya suluhisho la kukabiliana na maadui wa usalama wa Ulaya lazima lihusishe umoja huo katika kusaidia kidiplomasia na kifedha kumaliza mgogoro wa miaka mingi kati ya Israel na Palestina.
“Tumejifunza kutoka katika historia kuwa maamuzi magumu zaidi siku zote hufanyika wakati tuko katika ncha ya kutumbukia katika maangamizi. Ninaamini hapo ndipo tulipo hivi sasa: katika ncha ya maangamizi,” Borrell aliwaambai wabunge wa EU Jumatano.
“Ninaposikia mamlaka za dini ya Kiislam wakizungumza lugha ya mivutano ya kidini na wakiweka wazi kuwa Ulaya ni sehemu ya mgogoro huu, ninahisi kuwa wingu la kimbunga linakuja,” alisema.
Pia, siyo changamoto zote za Ulaya zinafungamana moja kwa moja na vita hivyo.
Mapema Alhamisi, Sweden ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa mawaziri kutoka nchi nane, kati ya hizo ni Ujerumani, Ubelgiji na Ufaransa, uliojikita katika kutaftua njia ya kukabiliana na matukio yanayo husisha watu kuchoma kitabua kitakatifu cha Waislam, Kuran.
Waendesha mashtaka wanajaribu kufahamu iwapo hilo lilikuwa kichocheo cha Mtunisia mmoja aliyewaua raia watatu wa Sweden huko Brussels Jumatatu, akiwauwa wawili kati yao, kabla ya mechi ya mpira wa miguu kati ya Ubelgiji na Sweden katika mji mkuu.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.
Forum