Kikundi cha wanamgambo wa Hezbollah kinachoungwa mkono na Iran kimeitisha kuwepo “Siku ya ghadhabu” Jumatano kwa ajili ya kulaani shambulizi hilo.
Kufuatia mlipuko wa Jumanne ambao Wizara ya Afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza ilisema uliuua watu 500, maandamano yamezuka katika maeneo mbalimbali nchini Lebanon, ikiwemo eneo la Ubalozi wa Ufaransa mjini Beirut na Ubalozi wa Marekani nje ya mji huo.
Waandamanaji walikusanyika pia nje ya ubalozi wa Israel huko Uturuki na Jordan, na pia ubalozi wa Ufaransa na Uingereza katika mji mkuu wa Iran na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tunisia.
Huko Ukingo wa Magharibi, majeshi ya Palestina yalitumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji ambao walipaza sauti zao kupinga utawala wa Rais Mahmoud Abbas.
Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.
Forum