Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi alisema siku ya Jumatano kwamba mamilioni ya Wamisri watapinga kulazimishwa kwa Wapalestina kuhamishwa hadi Sinai, na kuongeza kuwa hatua yeyote kama hiyo itaigeuza Peninsula hiyo kuwa eneo la mashambulizi dhidi ya Israeli.
Ukanda wa Gaza uko chini ya udhibiti wa Israel na Wapalestina badala yake wanaweza kuhamishwa hadi kwenye jangwa la Negev la Israel hadi wanamgambo hao watakaposhughulikiwa, Sisi aliuambia mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari mjini Cairo na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani.
Mpaka kati ya Rasi ya Sinai ya Misri na Ukanda wa Gaza ni eneo la kivuko pekee kutoka eneo la Palestina ambalo halidhibitiwi na Israel.
Mashambulio ya mabomu na kuzingirwa kwa Israel dhidi ya Gaza yamezusha hofu kwamba wakazi wake milioni 2.3 wanaweza kulazimishwa kuelekea kusini ndani ya Sinai.
Kinachotokea sasa huko Gaza ni jaribio la kuwalazimisha wakaazi kuchukua hifadhi na kuhamia Misri, jambo ambalo halipaswi kukubaliwa alisema Sisi.
Forum