Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:22

Biden awasili Israel wakati mzozo ukiongezeka kufuatia mlipuko kwenye hospitali ya Gaza


Rais wa Marekani Joe biden (Kulia), akiwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahi Jumatano mjini Tel Aviv. Oktoba 18,2023.
Rais wa Marekani Joe biden (Kulia), akiwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahi Jumatano mjini Tel Aviv. Oktoba 18,2023.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano amewasili Israel mzozo ukiwa umeongezeka sana  kufuatia mlipuko mkubwa kwenye hospitali huko Gaza, ambao umechochea shutuma kali sana za lawama na mandamano kote katika eneo hilo.

Wakati Biden anatarajiwa kukutana na viongozi wa Israel kuonyesha uungaji mkono wa muda mrefu kwa mshirika mkuu wa Marekani, mkutano muhimu na viongozi wa kiarabu ambao ulikuwa ufanyike Jordan umeakhirishwa kufuatia mlipuko huo.

Wanamgambo wa Hamas wameilaumu Israel kutokana na mlipuko katika hospitali ya Ahli Arab huko Gaza City, na kusema ‘ni uhalifu wa mauaji ya maangamizi, kwa mara nyingine tena unadhihirisha serikali katili na ya kigaidi.’

Taarifa ya utawala wa Palestina imesema waathirika wengi ni familia zisizokuwa na makazi, wagonjwa, watoto na wanawake, takriban watu 500 wempoteza maisha.

Jeshi la Israel la IDF kwa upande wake limedai kwamba roketi kutoka kwa wanamgambo wa Hamas ilipiga kwenye hospitali hiyo kwa makosa, dai ambalo Hamas imekanusha.

Forum

​
XS
SM
MD
LG