Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:15

Mlipuko kwenye hospitali ya Gaza unamsababisha Biden kuahirisha ziara ya Jordan


Rais wa Marekani Joe Biden akipanda ndege ya Air Force One kwenye uwanja wa Joint Base Andrews, Maryland, akielekea Israelon October 17, 2023.
Rais wa Marekani Joe Biden akipanda ndege ya Air Force One kwenye uwanja wa Joint Base Andrews, Maryland, akielekea Israelon October 17, 2023.

Rais Biden ameahirisha ziara yake ya Jordan akiwa njiani kuelekea Israel, baada ya mlipuko mkubwa kutokea kwenye hospitali moja mji wa Gaza City na kusababisha vifo vya mamia ya watu.

Rais Biden akiwa njiani kuelekea Mashariki ya Kati kujaribu kutafuta suluhisho la kusitisha ghasia zinazoendelea kati ya Israel na Hamas, ndipo serikali ya Jordan ilipotangaza kwamba mkutano wa kilele ulopangwa kufanyika Jumatano kati yake na viongozi wenzake wa Jordan, Misri na Palestina umeahirishwa.

Uwamuzi huo ulichukuliwa baada ya rais Mahamoud Abass wa Palestina kuamua kuondoka Amann ambako alipanga kuhudhuria mkutano huo akiwa amekasirishwa na shambulio dhidi ya hospitali inayosimamiwa na kanisa la batist mjini Gaza, la Al-Ahli Arab.

Wapalestina walojeruhiwa kutokana na shambulizi kwenye hospitali ya Al-Ahli Arab mjini Gaza.
Wapalestina walojeruhiwa kutokana na shambulizi kwenye hospitali ya Al-Ahli Arab mjini Gaza.

Kila upande katika vita hivyo vya Ukingo wa Gaza unamlaumu mwengine kwa mlipuko huo mkubwa ulotikisha hospitali ya Al-Ahli Arab, kwenye mji wa Gaza City na kusababisha vifo vya mamia ya watu.

Kundi la wanamgambo la Hamas kwenye taarifa Jumanne usiku, linailaumu Israel kwa shambulio dhidi ya hospitali hiyo, kikidai kwamba mamia ya watu walouliwa walikua wamepata hifadhi hapo, wakiwa ni familia, wagonjwa, watoto na wanawake. Maafisa wa Palestina wanasema zaidi ya watu 500 waliuliwa kutokana na shambulio hilo kubwa.

Kwa upande wake jeshi la Israel, IDF linakanusha kuhusika na shambulio hilo, likidai kwamba lilifanywa na kundi la wanamgabo la Islamic Jihad ambalo lilifyetua roketi ambayo haikufanikiwa kufyetuka kwenda mbali na kuangukia hospitali.

Kundi la Islamic Jihad limetoa taarifa likikanusha pia kuhusika na shambulio hilo.

Hapa Marekani, wizara ya ulinzi, Pentagon ilitoa taarifa ikisema kwamba haijapata bado uthibitisho juu ya nani alihusika na shambulio hilo lililotokea angani dhidi ya hospitali ya Al-Ahli Arab.

Hayo yakitokea White House ilitoa taarifa karibu na wakati ule ule ambao Rais Joe Biden anachukua ndege kuelekea Mashariki ya Kati, ikieleza kwamba Rais amesikitishwa na kukasirishwa sana baada ya kupata habari za shambulio hilo.

Taarifa inaeleza kwamba rais mara moja alituma rambi rambi zake kwa watu walouliwa ambao hawakua na makossa na kuwatakia walojeruhiwa afwen ya haraka.

Forum

XS
SM
MD
LG