Katika tamko hilo Marekani imeeleza kuwa imepokea taarifa za ukiukwaji wa taratibu na kanuni za uchaguzi huo kulikofanywa na wasimamizi wa uchaguzi kwa kiasi kikubwa na kuwatenga wagombea kutoka vyama vya Upinzani katika mchakato huo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa mkanganyiko huo unazua maswali kuhusu uhalali wa mchakato mzima wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Aidha katika Tamko hilo pia ubalozi wa Marekani umeeleza kusikitishwa kwake na msimamo wa Serikali ya Tanzania kukataa kutoa vibali kwa wakati kwa waangalizi wanaoukabalika na Mashirika yenye uzoefu na hivyo kuondoa imani kuwa mchakato huo ulikuwa halali .
Vyama vya upinzania nchini Tanzania vilisusia uchaguzi wa serikali za mitaa baada ya idadai kubwa ya wagombea wao kuenguliwa kushiriki katika uchaguzi huo.
Hata hivyo Serikali ya Tanzania imeelza kuwa hatua hiyo ilitokana na wagombea hao kushindwa kufuata tarataibu na kanuni za kuomba kuteuliwa kugombea katika uchaguzi uliofanyika tarehe 24 November mwaka huu