Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:39

Maiti zazagaa katika mitaa ya Derna, huku misaada ikimiminika Libya


Watu wanatembea katika vifusi, baada ya dhoruba kali na mvua kubwa huko Derna, Libya Septemba 12, 2023. Picha na REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Watu wanatembea katika vifusi, baada ya dhoruba kali na mvua kubwa huko Derna, Libya Septemba 12, 2023. Picha na REUTERS/Esam Omran Al-Fetori

Juhudi za misaada ya kimataifa kwa Libya zilishika kasi siku ya Alhamisi baada ya mafuriko makubwa kama ya tsunami kuua takriban watu 4,000, huku maelfu ya wengine hawajulikani walipo - idadi ya vifo ambayo UN imelaumu kuwa ni sehemu ya urithi wa miaka ya vita na machafuko.

Mawimbi makubwa ya maji ya dhoruba yalipasua mabwawa mawili ya juu ya mto Jumapili jioni na kuufanya mji wa Derna kuwa janga kubwa kama mwisho wa dunia, wakati ambapo mji mzima na idadi kubwa ya watu isiyohesabika kusombwa na maji hadi kwenye bahari ya Mediterranean

"Ndani ya sekunde chache maji yalipanda ghafla," alisimulia manusura mmoja aliyejeruhiwa ambaye alisema alisombwa na maji akiwa na mama yake katika mkasa huo wa usiku kabla ya wote wawili kufanikiwa kung'ang'ania na kuingia ndani ya jengo tupu ambapo mto ulikuwa ukiwapeleka.

Mamia ya mifuko yenye miili sasa imejaa katika mitaa ya Derna yenye matope, ikisubiri mazishi ya pamoja, huku wakazi waliojawa na kiwewe na majonzi wakiwatafuta ndugu zao waliopotea katika majengo yaliyoharibiwa na mabuldoza yakisafisha mitaa iliyo na vifusi na milima ya mchanga.

"Maafa haya yalikuwa ya vurugu na ya kikatili," alisema Yann Fridez, mkuu wa ujumbe wa Libya wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, ambayo ilikuwa na timu huko Derna wakati wa mafuriko.

"Wimbi lenye urefu wa mita saba liliosha majengo na kusomba miundo mbinu kuingia baharini. Sasa wanafamilia wamepotea, maiti zinarudishwa ufukweni na mawimbi na nyumba zimeharibiwa."

Libya sasa imegawanyika kati ya mamlaka mbili hasimu -- serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, inayotambulika kimataifa mjini Tripoli, na utawala ulio na makao yake mashariki iliyokumbwa na maafa.

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani Petteri Taalas amesema vifo vingi vingeweza kuepukika kama maonyo ya mapema na mifumo ya dharura ingefanya kazi ipasavyo katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.

Chanzo cha taariga hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG