Attaf ambaye hivi karibuni alifanya ziara katika nchi za Afrika Magharibi, alisema nchi nyingi alizozungumza nazo zinapinga uingiliaji kati wa kijeshi kumaliza mzozo huo.
Wakuu wa majeshi ya nchi wanachama wa ECOWAS walikutana nchini Ghana wiki iliyopita kujadili uwezekano wa uingiliaji kati wa kijeshi nchini Niger baada ya wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa rais kuchukua madaraka mwezi uliopita na kuweka uongozi wa kijeshi.
Algeria ilisema mara kadhaa kwamba inapinga uingiliaji kati wa kijeshi, ikitaja machafuko ambayo yalifuatia hatua ya NATO nchini Libya mwaka 2011 wakati wa uasi dhidi ya kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi.
Attaf alisema maafisa wa Algeria wamezungumza mara tatu na kiongozi wa mapinduzi nchini Niger tangu mapinduzi, ambaye naye pia anataka utawala wa mpito wa hadi miaka mitatu.
Forum