Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:47

Maelfu ya watu wanaaminika wamefariki kutokana na mafuriko nchini Libya


Picha hii iliyotolewa na Shirika la Mwezi mwekundu nchini Libya Septemba 11, 2023, inaonyesha wafanyakazi wake wakifanya kazi kufungua barabara zilizokumbwa na mafuriko katika eneo lisilojulikana mashariki mwa Libya.
Picha hii iliyotolewa na Shirika la Mwezi mwekundu nchini Libya Septemba 11, 2023, inaonyesha wafanyakazi wake wakifanya kazi kufungua barabara zilizokumbwa na mafuriko katika eneo lisilojulikana mashariki mwa Libya.

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko nchini Libya inaweza kufikia maelfu, afisa kutoka Shirikisho la kimataifa la msalaba mwekundu na Mwezi Mwekundu (IFRC) amewaambia waandishi wa habari leo Jumanne.

“Idadi ya waliofariki ni kubwa,” amesema Tamer Ramadan, mkuu wa ujumbe wa IFRC nchini Libya.

Ramadan amesema shirika lake limethibitisha kutoka vyanzo huru kwamba kuna watu 10,000 hawajulikani walipo.

Maafisa mashariki mwa Libya walisema Jumatatu kwamba takriban watu 2,000 wanaaminaka walifariki katika mji wa Derna.

Eneo hilo lilikumbwa na mvua kubwa na mafuriko kutokana na kimbunga Daniel kutoka Mediterranean, na kusababisha mabwawa kupasuka na vitongoji vyote kusombwa na maji.

Video iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha mitaa imegeuka mito iliyofurika katika miji ya Derna pamoja na Benghazi, Sousse, Al Bayda na Al-Marj.

Forum

XS
SM
MD
LG