Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:24

Waziri wa mambo ya kigeni wa Libya asimamishwa kazi kutokana na kukutana na mwenzake wa Israel


Waziri wa mambo ya kigeni wa Libya, Najla Mangoush, aliyesimamishwa kazi Jumapili.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Libya, Najla Mangoush, aliyesimamishwa kazi Jumapili.

Waziri mkuu wa Libya Jumapili amemsimamisha kazi waziri wa mambo ya kigeni Najla Mangoush na kuamuru achunguzwe baada ya Israel kusema kwamba alikutana na waziri wake wa mambo ya kigeni Eli Cohen wiki iliyopita, licha ya mataifa yao kutokuwa na uhusiano rasmi wa kidiplomasia.

Cohen alisema kwamba walizungumza na Mangoush kuhusu umuhimu wa kudumisha turathi za kiyahudi nchini Libya. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, taarifa ya Israel kuhusu mkutano huo uliofanyikia Italy zilipelekea maandamano madogo nchini Libya, ambayo haitambui Israel.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Libya imesema kwamba Mangoush alikuwa amekataa kufanya mkutano na wawakilishi wa Israel, na kwamba kilichpofanyika ni kwamba walikutana nao bila kukusudia kwenye ofisi za wizara ya mambo ya kigeni ya Italy.

Taarifa hiyo imeongeza kusema kwamba mawaziri hao hawakuwa na mazungumzo ya aina yoyote, na kwamba Libya inaendelea kukataa kurejesha uhusiano wake na Israel. Tangu 2020, Israel imejitahidi kurejesha ushusiano wake na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, Bahrain, Morocco na Sudan, kupitia mkataba maarufu kama Abraham accords, iliosimamiwa na Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG