Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:17

Umoja wa Mataifa: Vifo vingi vingeepukwa Libya ikiwa onyo la mifumo ya usimamizi wa dharura ingefanya kazi


Magari yamerundikana juu ya vifusi vya jengo lililoharibiwa na mafuriko baada ya dhoruba ya Mediterania "Daniel" kupiga mji wa mashariki mwa Libya wa Derna, Septemba 14, 2023.
Magari yamerundikana juu ya vifusi vya jengo lililoharibiwa na mafuriko baada ya dhoruba ya Mediterania "Daniel" kupiga mji wa mashariki mwa Libya wa Derna, Septemba 14, 2023.

Maoni haya yalikuja baada ya mafuriko makubwa yenye ukubwa wa tsunami kupiga mashariki mwa Libya mwishoni mwa juma, na kuua takriban watu 4,000, huku maelfu wengine wakipotea na kuhofiwa kufariki dunia

Umoja wa Mataifa ulisema siku ya Alhamisi kwamba maelfu zaid ya vifo katika janga la mafuriko nchini Libya vingeweza kuepukika ikiwa onyo la mapema na mifumo ya usimamizi wa dharura ungefanya kazi ipasavyo.

Kwa uratibu bora wa utendaji katika nchi iliyokumbwa na mzozo, wangeweza kutoa maonyo na vikosi vya usimamizi wa dharura vingeweza kutekeleza uhamishaji wa watu, na tungeweza kuzuia vifo vingi, Petteri Taalas mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani la Umoja wa Mataifa, aliwaambia wanahabari mjini Geneva.

Maoni yake yalikuja baada ya mafuriko makubwa yenye ukubwa wa tsunami kupiga mashariki mwa Libya mwishoni mwa juma, na kuua takriban watu 4,000, huku maelfu wengine wakipotea na kuhofiwa kufariki dunia

Forum

XS
SM
MD
LG