Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:13

Wahamiaji wanne wazama Ugiriki walipokuwa wakijaribu kuvuka bahari

Wahamiaji wakiwa wamepanda boti wakijaribu kuingia Ugiriki. Picha na Ozan KOSE / AFP.
Wahamiaji wakiwa wamepanda boti wakijaribu kuingia Ugiriki. Picha na Ozan KOSE / AFP.

Ugiriki ni mojawapo ya sehemu kuu za Umoja wa Ulaya  kwa wahamiaji na wakimbizi wanaokimbia umaskini na migogoro huko Mashariki ya Kati, Afrika na Asia.

Wahamiaji wanne walizama kwenye kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos walipokuwa wakijaribu kuvuka bahari kutoka nchi jirani ya Uturuki walinzi wa pwani walisema Jumatatu na kuongeza kuwa wengine 18 waliokolewa. Walinzi hao hawakutoa maelezo zaidi.

Ugiriki ni mojawapo ya sehemu kuu za Umoja wa Ulaya kwa wahamiaji na wakimbizi wanaokimbia umaskini na migogoro huko Mashariki ya Kati, Afrika na Asia.

Zaidi ya watu 15,600 wamewasili Ugiriki mwaka huu kwa mujibu wa taarifa za UNHCR karibu 12,000 kati yao kwa njia ya Bahari.

Mwezi Juni mamia ya watu walizama katika maji ya kimataifa karibu na Ugiriki baada ya meli ya uvuvi waliyokuwa wakisafiria kuzama ilipokuwa ikielekea Italia kutoka Libya.

Forum

XS
SM
MD
LG