Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:10

Kimbunga Chaua watu 150 Libya


Magari yanapita kwenye mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. Oktoba 19, 2022. Picha na Mahmud TURKIA / AFP.
Magari yanapita kwenye mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. Oktoba 19, 2022. Picha na Mahmud TURKIA / AFP.

Takriban watu 150 waliuawa katika mafuriko yaliyotokea mashariki mwa Libya kutokana na dhoruba ya kimbunga Daniel ambacho kimepiga katika bahari ya Mediterania, afisa mmoja alisema Jumatatu.

Picha zilizochukuliwa na wakazi wa eneo la maafa, zilionyesha maporomoko makubwa ya matope, majengo yaliyoanguka na vitongoji vyote vilivyozama chini ya maji.

Shirika la habari la Reutes limeripoti kuwa, picha zilizoonekana kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakiwa wamekwama juu ya magari yao wakati wakijaribu kupata msaada katika mafuriko hayo makubwa, wakati kimbunga Daniel kikipiga miji ya Benghazi, Sousse, Al Bayda, Al-Marj na Derna.

Wanajeshi saba wa Jeshi la Taifa la Libya hawajulikani walipo, msemaji wa jeshi hilo Ahmad Mesmari alisema.

“Tulikuwa tumelala, tulipoamka tuliona maji yamezingira nyumba. Tuko ndani na tunajaribu kutoka," mkazi mmoja wa eneo la Derna Ahmed Mohamed aliliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu, siku ya Jumatatu.

Shughuli za utafutaji na uokoaji zilikuwa zikiendelea, mashahidi alisema. Mamlaka zilitangaza hali ya mbaya ya hatari, na kufunga shule na maduka pamoja na kuweka amri ya kutoktoka nje.

Bandari kuu nne za mafuta za Ras Lanuf, Zueitina, Brega na Es Sidra, nchini Libya, zilifungwa kuanzia Jumamosi jioni kwa siku tatu, wahandisi wawili wa mafuta waliliambia shirika la habari la Reuters.

Wataalamu wamekitaja kimbunga Daniel -- ambacho pia siku za za hivi karibuni kiliyakumba maeneo ya Ugiriki, Uturuki na Bulgaria na kuua watu wasiopungua 27 – kutokana na “kiwango kibubwa cha mvua yalichonyesha katika muda wa saa 24".

Mamia ya wakazi wa maeno hayo wanasadikiwa bado wamekwama katika maeneo ambayo ni magumu kufikiwa wakati waokoaji wanaosaidiwa na jeshi wakijaribu kuwasaidia.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters/ AFP

Forum

XS
SM
MD
LG