Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:32

Libya yatuma ombi kwa Lebanon la kumuachilia mwana wa kiume wa Gadhafi


Mtoto wa kiume wa Moammar Gadhafi, Hannibal Gadhafi, ambaye anashikiliwa Lebanon. Picha ya maktaba.
Mtoto wa kiume wa Moammar Gadhafi, Hannibal Gadhafi, ambaye anashikiliwa Lebanon. Picha ya maktaba.

Mamlaka za kisheria nchini  Libya zimewasilisha  ombi rasmi kwa Lebanon kumuachilia  mmoja wa watoto wa kiume wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo Mommar Gadhafi

Mamlaka za kisheria nchini Libya zimewasilisha ombi rasmi kwa Lebanon kumuachilia mmoja wa watoto wa kiume wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo Mommar Gadhafi, Hannibal Gadhafi.

Hannibal Gadhafi alifungwa jela bila kufunguliwa mashitaka tangu 2015, na maafisa wa afya wamesema kwamba ombi hilo ni kutokana na kuzorota kwa afya yake. Ripoti zimeongeza kuwa afya yake ilianza kuzorota tangu alipoanza kususia chakula hapo Juni 3, akipinga kuwekwa jela bila kufunguliwa mashtaka.

Tangu wakati huo amepelekwa hospitali mara mbili , na amekuwa akinywa maji pekee. Kulingana na maafisa wawili wa mahakama wa Lebanon, mwendesha mashtaka mkuu wa Libya Al Sediq al Sour alituma ombi mapema mwezi huu kwa mwenzake wa Lebanon Ghassan Queidat, kuhusu kuachiliwa kwa Hannibal Gadhafi.

Ombi hilo lilisema kwamba iwapo Lebanon itatoa ushirikiano, basi ukweli kushusu hatma ya kiongozi mashuhuri wa kidini wa kishia wa Lebanon Moussa al Sadr aliyetoweka akiwa Libya 1978 utajulikana.

Forum

XS
SM
MD
LG