Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 07:05

Leila Sheikh mwanaharakati wa uhuru wa vyombo vya habari Tanzania afariki dunia


Leila Sheikh Hashim, mwandishi habari, mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto Tanzania
Leila Sheikh Hashim, mwandishi habari, mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto Tanzania

Tasnia ya habari nchini Tanzania inaomboleza kifo cha mwandishi wa habari mkongwe na mmoja wa waanzilishi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Leila Sheikh ambaye alifariki ghafla usiku wa kuamkia Jumatatu. Chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana.

Leila aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji na miongoni mwa waanzilishi wa Chama cha Waandishi Habari Wanawake Tanzania, TAMWA, kuanzia mwaka 1996 hadi 2001.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dk. Rose Reuben ameiambia Sauti ya Amerika kuwa kifo cha Leila kimewashtua watu wengi siyo tu katika tasnia ya habari lakini pia katika sekta nyingine.

"Alikuwa akifanya kazi zake kama kawaida mpaka siku ya mwisho, “nimesoma ujumbe wake wa mwisho ambao alikuwa ameutuma kwenye kundi lake la WhatApp saa moja na dakika 40 jioni” amesema Dk. Ruben.

Ujumbe wake wa mwisho alioutuma kwenye kundi lake la ‘Women Matters” ulihusu filamu kuhusu madhara ya biashara haramu ya ngono nchini Marekani.

Leila Sheikh alikuwa mwanablogu, mwanaharakati na mtetezi wa haki za wanawake na watoto, na mhariri wa gazeti la Sauti ya Siti lililochapishwa na TAMWA.

Sauti ya Amerika inatuma salaam za rambi rambi kwa familia, jamaa na marafiki wa Leila ambaye pia alikuwa mmoja kati ya wachambuzi wa Idhaaa ya Kiswahili ya VOA wa masuala mbali mbali ikiwa ni pamoja na masuala ya wanawake, watoto na uandishi habari.

Leila atazikwa siku ya Jumanne katika makaburi ya Mabawa, Tanga.

Forum

XS
SM
MD
LG