Waziri wa Nishati January Makamba amesema uidhinishwaji wa mikataba ya mradi huo ambao umechelewa kwa muda mrefu- inalenga uchimbaji wa rasilimali kubwa ya gesi iliyoko nchini lakini asilimali iko baharini – mikataba hiyo itawasilishwa katika baraza la mawaziri kabla ya kusainiwa.
Wakati huo huo Makamba hakutoa muda maalum katika maelezo yake bungeni, hotuba ya bajeti ya wizara ya nishati kwa mwaka 2023/24 iliyochapishwa katika tovuti yake ilionyesha kuwa mwezi Juni wawekezaji wa LNG na serikali wanatarajiwa kusaini makubaliano ya ushirikiano wa uzalishaji uliofanyiwa marekebisho.
"Mradi huo wa dola bilioni 42 utabadilisha taswira na sura ya uchumi wetu,” alisema Makamba na kuongeza kuwa serikali itatunga sheria maalum ya kufuatilia mradi huo.
Mapema mwezi huu, makampuni ya Equinor, Shell na Exxon Mobil walisema wamefikia makubaliano na nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kuendeleza kituo cha mauzo ya nje cha LNG.
Tangu aingie madarakani mwaka 2021, Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akiweka msukumo katika ukamilishaji wa mashauriano hayo ambayo yamechelewesha mradi huo kwa muda mrefu. Mradi wa LNG ulikuwa ulikwama kwa muda wa miaka saba.
Chanzo cha habari ni shirika la habari la Reuters.
Forum