Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:05

Fulgence Kayishema amekamatwa akiwa Afrika kusini


Fulgence Kayishema
Fulgence Kayishema

Kayishema ni  inspekta wa zamani wa polisi anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari, kushirikiana na kupanga njama za kutenda mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa leo Alhamisi wamesema kuwa Fulgence Kayishema mmoja wa watoro wanne ambao walikuwa wakitafutwa kwa jukumu lao katika mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994 amekamatwa nchini Afrika Kusini. Mahakama ya Kimataifa ya kwa Kesi za Uhalifu (MICT) alisema katika taarifa kwamba Kayishema alikamatwa huko Paar, Afrika Kusini katika operesheni ya pamoja.

Amekuwa akikwepa sherika tangu Julai 2001, kwa mujibu wa tovuti ya MICT. Yeye na wenzake wanashutumiwa kwa mauaji ya zaidi ya watutsi 2,000 wanaume, wanawake na watoto ambao walichukua hifadhi katika kanisa katoliki huko Nyange katika wilaya ya Kivumu.

“Kayishema moja kwa moja alishiriki katika kupanga na kutenga mauaji haya, ikiwemo kupata na kusambaza petrol ili kulichoma kanisa likiwa na wakimbizi ndani”, ilisema taarifa.

“Wakati hili liliposhindwa, Kayishema na wenzake walitumia bulldoza ili kulivunja kanisa, kuwazika na k uwaua wakimbizi waliokuwa ndani.

“kayishema na wenzake walisimamia kuhamishwa kwa miili kutoka kwenye ardhi ya kanisa na kuzikwa kwenye kabura la jumla katika kipindi cha takriban siku mbili,”

“MICT ambayo makao makuu yake yako The Hague na Arusha, Tanzania mwaka 2015 ilichukua kazi za Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa Rwanda (ICTR) ambayo Umoja wa Mataifa iliiunda kufuatilia mauaji ya kimbari.

Alikamatwa katika operesheni ya pamoja iliyofanywa timu ya kufuatilia watoro ya MICT na mamlaka za Afrika Kusini taarifa ilisema. Fulgence Kayishema alikuwa mtoro kwa zaidi ya miaka 20. Kukamatwa kwake kunahakikisha hatimaye haki itapatikana kwa uhalifu anaoshutumiwa aliutenda,” mwendesha mashtaka mkuu wa MICT Serge Brammertz alisema katika taarifa.

Forum

XS
SM
MD
LG