Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:06

Baadhi ya wafanyabiashara wadai kuendelea na mgomo Kariakoo


Soko la Kariakoo, Dar es Salaam, Tanzania.
Soko la Kariakoo, Dar es Salaam, Tanzania.

Baadhi ya maduka katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania huenda yakaendelea kufungwa kufuatia mgomo wa wafanyabiashara wanaopinga rushwa na malimbikizo ya kodi wanayotozwa na Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania (TRA).

Mgomo huo ambao ulifanyika siku ya Jumatatu umekuwa na mgawanyiko miongoni mwa wafanyabiashara ambao baadhi yao wameelezea msimamo wa kuendelea na mgomo mpaka watakapo kutana na rais Samia Suluhu Hassan ili aweze kutatua changomoto wanazopitia.

Katibu wa jumuiya ya wafanyabiashara katika mkoa wa Dar-es -Salaam Riziki Ngaga akizungumza na Sauti ya Amerika amesema licha ya mkuu wa mkoa huo Amosi Makala pamoja wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzungumza na wafanyabiashara hao, kuna baadhi wamedai kuwa wataendelea na mgomo mpaka watakapokutana na rais Samia.

“Lakini wafanyabiashara wanaelezea kuwa wataendelea na mgomo mpaka hapo rais atakapoingilia kati suala hili” alisema Ngaga.

Wafanyabiashara hao wamekuwa wakitumia makundi katika mitandao ya kijamii kama vile WhatApp wakidai kuendeleza mgomo wakiwa wamepiga picha huku wameshikiria mabango ya kutaka kuonana na rais, wakati mabango mengine yakiwemo mitaani, alisema Ngaga.

Lakini baadhi yao huenda wakafungua biashara zao baada ya kukutana na waziri mkuu. Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo wadogo “Wamachinga” katika soko la Kariakoo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa wafanyabiashara hao nchini Tanzania Idd Lusinde, amesema.

Miongoni mwa sababu zilizopelekea wafanyabiashara hao kugoma ni mrundikano wa kodi zinazotozwa na mamlaka ya mapato Tanzania TRA pamoja na rushwa zinazobabisha na ukosefu wa malipo elekezi ya kodi kwa bidhaa zinazoingizwa kutoka nchi za nje na kuuzwa kwenye soko hilo.

Ukosefu wa kiwango elekezi cha ushuru wakati wa utoaji wa bidhaa hizo bandarini husababisha rushwa kwa kuwa mfumo wa utozaji kodi ni wa majadiliano, kwa hiyo “rushwa muda mwingine inakuwa kubwa kuliko kodi yenyewe”, alisema Ngaga.

Wakati wa mkutano wake na wafanyabiashara hao Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahidi kuendelea kutatua changamoto zinazowaketa wafanyabiashara hao.

Hata hivyo Waziri Mkuu huyo ameiagiza TRA kusitisha Matumizi ya Kikosi Maalum "Task Force" ambacho kilikuwa kinaendesha zoezi la ukamataji wa wafanyabiashara katika soko hilo la Kariakoo.

MARIAM MNIGA, SAUTI YA AMERIKA, WASHINGTON DC.

XS
SM
MD
LG