Viongozi mbalimbali wametembelea eneo hilo wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ambaye ameagiza uchunguzi huo kufanyika ndani ya siku saba.
Pia Majaliwa ameahidi kuwa serikali itazungumza na mabenki yaliyo wakopesha Wafanyabiashara waliounguliwa na maduka yao.
Aidha changamoto ya vifaa kwa Idara ya Zimamoto pamoja na miundombunu hafifu katika eneo hilo vinaelezwa kuchangia pakubwa athari zaidi za moto huo ulioanza kuwaka majira ya saa moja jioni Jumamosi tarehe 10 na kuteketeza maduka na mali za wafanyabiashara katika soko hilo.
Tathmini halisi ya hasara iliyosababisha na moto huo itatolewa baada ya uchunguzi wa tume iliyoundwa na ofisi ya waziri Mkuu kukamilisha kazi hiyo katika kipindi cha siku saba.
Kwa sasa eneo hilo linallindwa na jeshi la polisi kwa lengo la kulinda mali zilizonusurika hadi pale itakapoatangazwa vingine.