Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:07

Ajali mbaya ya magari Algeria yaua watu 27


Ramani ikionyesha Algeria
Ramani ikionyesha Algeria

Watu wasiopungua 27 wamefariki katika ajali mbili mbaya za magari Ijumaa usiku, vyombo vya habari nchini Algeria vimeeleza.

Katika ajali mmoja basi liligongana na lori kwenye barabara inayounganisha mji wa Constantine na mji wa bandari wa Jijel kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Ajali hiyo ili sababisha vifo vya watu 18 na 11 kujeruhiwa, taarifa hiyo imeeleza.

Watoto sita ni miongoni mwa wale waliofariki kulingana na shirika rasmi la habari la Algeria APS.

Wakati huohuo katika ajali nyingine kusini mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Mali watu tisa waliuawa wakati gari la pickup walilokuwa wakisafiri nato lilipogongana na lori kutokana na hali mbaya ya hewa.

Taarifa inasema ajali hiyo ilitokana na ukungu ambao uliwiya vigumu madereva kuona vizuri barabarani.

Chanzo cha Habari cha Algeria : APS

XS
SM
MD
LG