Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:05

Baraza la Usalama launga mkono juhudi za upatanishi za AU


FILE - Mto Blue Nile ukitirika kuelekea katika bwawa la Grand Ethiopian Renaissance karibu na Assosa katika mkoa wa Benishangul-Gumuz wa Ethiopia, karibu na Sudan, takriban kilomita 800(maili 500) kutoka Addis Ababa.
FILE - Mto Blue Nile ukitirika kuelekea katika bwawa la Grand Ethiopian Renaissance karibu na Assosa katika mkoa wa Benishangul-Gumuz wa Ethiopia, karibu na Sudan, takriban kilomita 800(maili 500) kutoka Addis Ababa.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameunga mkono juhudi za upatanishi za Umoja wa Afrika katika kutanzua mzozo wa bwawa kwenye Mto Nile kati ya Ethiopia Sudan na Misri.

Baada ya kikao cha Alhamisi Baraza la Usalama lilizitaka nchi hizo tatu kuanza tena majadiliano yao ambayo hadi hivi sasa hayajaweza kuleta mafanikio muhimu tangu yalipoanza karibu miaka 10 iliyopita.

Mkutano huo wa Baraza la Usalama uliitishwa na Misri na Sudan kutokana na kile walichokieleza ni kitisho muhimu kinachowakabili wananchi wa nchi hizo mbili kutokana na Bwawa la Ethiopia la Grand Ethiopian Renaissance Dam, GERD.

Mvutano umeongezeka tangu Jumapatu, pale Addis Ababa ilipotangaza imeanza awamu ya pili ya kujaza maji kwenye bwawa hilo.

Mjumbe maalum wa Katibu mkuu kwa ajili ya nchi za Pembe ya Afrika Parfait Onanga Anyanga aliwaambia wajumbe wa Baraza la Usalama kwamba licha ya juhudi mbalimbali za upatanishi Ethiopia, Sudan na Misri hazijaweza kukubaliana kutanzua matatizo yaliyobaki.

Parfait Onanga-Anyanga
Parfait Onanga-Anyanga

Anyanga ameeleza : "Tuna amini kwa pamoja pamoja na washirika wenu kuna nafasi ya kusonga mbele katika kutanzua matatizo yanayohusiana na GERD kwa njia ya amani na maelewano."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry amelitaka Baraza la Usalama kuzihimiza nchi hizo tatu kufikia makubaliano katika muda wa miezi sita ijayo juu ya matumizi ya maji ya Mto Nile.

Shoukry amesema : "Bw Rais Misiri ni taifa la zaidi ya watu milioni 100 linakabiliwa na kitisho kikubwa. Ujenzi wa ukuta mkubwa wa vyuma umefanyika kwenye ukingo wa mto mkubwa wa kale na umezusha wingu zito katika mustakbal na hatma ya watu wa Misri.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Demeke Mekonnen, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry, na Waziri wa Mambo ya Nje wa SudanAsma Mohamed Abdalla walipokutana Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Demeke Mekonnen, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry, na Waziri wa Mambo ya Nje wa SudanAsma Mohamed Abdalla walipokutana Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa upande wake Waziri wa Maji na Nishati wa Ethiopia Seleshi Bekele Awulachew anasema wanakabiliana na mradi wa kuzalisha umeme kwenye bwawa ambao si wa kwanza barani Afrika au kwengineko duniani.

Bekele anaeleza : Kwa kukuarifu bwawa la GERD ni mara mbili na nusu dogo kuliko bwawa la Aswan nchini Misri. Pengine kinachotofautisha GERD na miradi mingine ni kiwango cha matumaini na matarajio kilichopewa watu wa Ethiopia milioni 65 ambao hawana umeme. na pia ni tofauti na ya kipekee kwa sababu ujenzi wa mradi huo wenye thamani ya dola bilioni 5 umegharimiwa na damu, machozi na jasho la Waethiopia wa kawaida.

Asilimia 80 ya mradi huo imekamilika na unatarajiwa kuanza kuzalisha umeme kwa ukamilifu hapo mwaka 2023 na kuifanya kuwa kinu kikubwa kabisa cha umeme barani Afrika na cha saba duniani.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan ameliambia baraza huu ni wakati wa kipekee kuwahi kutokea kwa bazara hilo kuchukua jukumu la kidiplomasia kuzuia mgogoro na wala si kupeleka walinda amani.

Mariam Sadiq al-Mahdi, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Sudan ameeleza : "Lakini ni juhudi za kidiplomasia kuepusha mgogoro kwa kuzingatia ishara za awali na kuchukua hatua za mapema kujenga uaminifu, kujenga uaminifu katika jumuia muhimu sana ya kikanda kama Umoja wa Afrika. Pamoja na kujenga uaminifu kati ya nchi muhimu kama vile Sudan, Ethiopia na Misri.

Sudan inataka baraza la usalama kusaidia kupendekeza makubaliano yanayo hitajika kutekelezwa na pande zote na wala sio pendekezo la Tunisia lililowasilishwa na Misri la makubaliano kufikiwa katika muda wa miezi sita.

Vyanzo vya Habari : AFP / AP

XS
SM
MD
LG