Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:42

Ethiopia yaarifu Misri kuhusu kujaza bwawa maji


Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance Dam, GERD, lililoko Guba, Ethiopia
Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance Dam, GERD, lililoko Guba, Ethiopia

 Waziri wa umwagiliaji maji wa Misri Mohamed Abdel Aty, Jumatatu amesema kuwa amepokea taarifa rasmi kutoka serikali ya Ethiopia kwamba imeanza tena kujaza maji kwenye bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Grand Ethiopian Renaissance Dam, GERD

Shirika la habari la Reuters linasema kuwa zoezi hilo sasa linafanyika kwa mwaka wa pili. Ethiopia inasema kuwa bwawa hilo ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi kutokana na umeme utakaozalishwa kwa wakazi wake.

Misri na Sudan wamekuwa wakilalamikia kuwa mradi huo ni tishio kwa vile utapunguza kiwango cha maji ya mto Nile ambayo yanategemewa sana kwenye mataifa hayo mawili.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya kikao Jumanne, waziri Aty akiwa ameliandikia barua baraza hilo kuhusiana na hatua ya karibuni ya Ethiopia kuendelea kujaza maji kwenye bwawa hilo.

Balozi wa Ethiopia nchini Sudan amesema Jumapili kwamba Sudan na Misri walifahamu kuhusiana na miaka mitatu ya kwanza ya kujaza bwawa hilo maji, na kwamba hakuna haja ya kulihusisha baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa kuwa sio mzozo wa kiusalama.

XS
SM
MD
LG