Misri inasema Ethiopia imeanza kujaza hifadhi ya maji ya bwawa lenye utata kwenye mto Nile. Hatua hiyo itaongeza mivutano katika Pembe ya Afrika kabla ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili mzozo huo, ambao pia unajumuisha Sudan.
Misri inasema inapinga vikali hatua hiyo ya upande mmoja. Inasema hatua hiyo ni tishio kwa usalama na amani ya eneo hilo.
Mzozo huo sasa unalenga jinsi gani Ethiopia inapaswa kujaza haraka hifadhi hiyo na ni kiasi gani cha maji itakayotoa kwa upande wa chini ikiwa kuna ukame wa miaka mingi. Misri na Sudan zimetoa wito mara kwa mara kwa Marekani, Umoja wa Mataifa, na Umoja wa Ulaya kusaidia kufikia makubaliano ya kisheria ambayo yangeelezea kinaga ubaga jinsi bwawa hilo litakavyoendeshwa na kujazwa.