Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 09:41

Soko la Kariakoo laungua moto


Soko la Kariakoo kabla ya ajali ya moto.
Soko la Kariakoo kabla ya ajali ya moto.

Soko kubwa nchini Tanzania la Kariakoo lililopo jijini Dar es Salaam limeteketea kwa moto uliozuka kuanzia majira ya saa tatu usiku kwa saa za Tanzania.

Moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana ulianza katika eneo la paa la juu la soko hilo na baadaye kuendelea kusambaa katika maeneo mengine.

Ingawa kulikuwa na juhudi za kuuzima moto huo hata hivyo kazi hiyo imeonekana kuwa ngumu sana kutokana na mazingira ya eneo hilo.

Jirani mmoja ambaye amezungumza na VOA amesema moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme iliozuka karibu na soko hilo.

Taarifa zaidi zinasema ingawa idara ya zimamoto ilifika katika eneo la tukio lakini hadi sasa imeshindwa kuuzima moto huo.

Baadhi ya watu walioshuhudia wanasema gari la zimamoto lilifika eneo la tukio na lilionekana kuishiwa na maji. Zimamoto nyingine kutoka mamlaka ya bandari imeitwa kwenda kusaidia juhudi za kuuzima moto huo.

Taarifa za awali zinasema moto huo unaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa mali ya mamilioni hasa kwa vile soko hilo limekuwa likitoa huduma karibu nchi nzima ya Tanzania na nchi jirani.

Hivi karibun Rais Samia Suluhu Hassan alifanya ziara katika soko hilo na aliahidi kulifanyia marekebisho na kullifanya kuwa la kisasa zaidi.

Soko la Kariakoo licha ya kuajiri wafanyabiashara wengi lakini ni kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki.

XS
SM
MD
LG