Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:56

Maandamano Kenya dhidi ya bei za bidhaa za duka la China Square


Picha ya eneo la biashara la Eastleigh Nairobi, Kenya Mei 6, 2020. Picha na shirika la habari la REUTERS/Thomas Mukoya/maktaba
Picha ya eneo la biashara la Eastleigh Nairobi, Kenya Mei 6, 2020. Picha na shirika la habari la REUTERS/Thomas Mukoya/maktaba

Zaidi ya wafanya biashara 1,000 nchini Kenya waliandamana katika mji kuu wa Nairobi Jumanne dhidi ya duka jipya la rejareja linalomilikiwa na raia wa China, wakilituhumu duka hilo kwa kuuza bidhaa kwa bei ya chini sana.

Wafanyabiashara nchini Kenya na mataifa mengine ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi barani Afrika, mara kwa mara wamekuwa wakifanya maandamano dhidi ya washindani wao wa kichina.

Wafanyabiashara nchini Kenya wamekasirishwa na duka jipya la reja reja la China Square lililofunguliwa nje kidogo ya jiji la Nairobi, ambapo bei za bidhaa za kila siku kama vile mapazia yaliyoingizwa kutoka China, huuzwa kwa bei nafuu ya wastani wa asilimia 50 kuliko yale yanayouzwa na wafanya bishara wa ndani.

China ni mshirika mkuu wa kibiashara barani Afrika na zaidi ya Wachina milioni moja wanakadiriwa kuishi barani humo.

Uhusiano wa Kenya na China ulizua mjadala wakati wa uchaguzi wa mwisho wa urais uliofanyika mwaka jana, ambao ulimpa ushindi William Ruto.

XS
SM
MD
LG