Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 12:17

Jill Biden atembelea miradi ya wanawake kwenye kitongoji cha Kibera jijini Nairobi

Jill Biden akiandamana na mke wa rais wa Kenya Rachel Ruto kwenye kitongoji cha Kibera Jumapili. Feb 25, 2023
Jill Biden akiandamana na mke wa rais wa Kenya Rachel Ruto kwenye kitongoji cha Kibera Jumapili. Feb 25, 2023

Mke wa Rais wa Marekani, Jill Biden, Jumapili ametembelea kitongoji cha Kibera mjini Nairobi, na kukutana na wanawake wanaojiwezesha kwa kutumia mpango wa kukopeshana fedha.

Chini ya mfumo huo, wanawake ambao mara nyingi hawana uwezo wa kupata mikopo kutoka kwa taasisi za fedha, hukopa pesa walizokusanya pamoja.

Wanawake hao ni wanachama wa kundi la Kibera's Table Banking linalofanyakazi kuwawezesha wanawake kukopa fedha ili waweze kutekeleza miradi yao.

Hii inawawezesha wanawake kuanzisha au kuendeleza biashara zao wenyewe, kukidhi gharama za nyumbani na hata kuwekeza katika elimu ya watoto wao.

Mke wa rais wa Marekani akifuatana na mwenzake Rachel Ruto wahudhuria kazi za kundi la wanawake kwenye kanisa la AP Community katika kitongoji cha Kibera.
Mke wa rais wa Marekani akifuatana na mwenzake Rachel Ruto wahudhuria kazi za kundi la wanawake kwenye kanisa la AP Community katika kitongoji cha Kibera.

Jill Biden amehimiza wanawake nchini Kenya kujihusisha zaidi katika uwekezaji na kuwataka kuendelea kusaidiana ili waweze kuzisaidia familia zao.

Baada ya kushuhudia jinsi makundi ya wanawake yanavyoweka pesa, mke wa Rais wa Marekani ametaja juhudi hizo kuwa za kuvutia na dhihirisho la uthabiti wa wanawake katika kujiimarisha kiuchumi.

Wanawake katika kikao hicho walionyesha utaratibu unaofuatwa katika kukopa na kuweka akiba kupitia vikundi vyao huku Jill Biden akitazama.

Mke wa rais wa Marekani akifuatana na mwenzake Rachel Ruto wahudhuria kazi za kundi la wanawake kwenye kanisa la AP Community katika kitongoji cha Kibera.
Mke wa rais wa Marekani akifuatana na mwenzake Rachel Ruto wahudhuria kazi za kundi la wanawake kwenye kanisa la AP Community katika kitongoji cha Kibera.

Jill Biden yupo nchini Kenya kwa ziara rasmi inayotarajiwa kuimarisha uhusiano ulio ulioimarika kati ya nchi hizo mbili, uwezeshaji wa wanawake na vijana na uhifadhi wa mazingira na uhaba wa njaa kama ajenda yake kuu.

Safari hiyo inajiri miezi michache baada ya Rais Joe Biden kuwakaribisha viongozi wa Afrika mjini Washington na kuahidi kwamba Marekani iko tayari kushiriki katika kuimarisha mustakabali wa Afrika. Hii ni ziara ya sita ya Dk. Biden barani Afrika, ziara ya kwanza nchini Namibia, na ziara ya tatu nchini Kenya.

Aidha Safari yake inafuatia ile ya waziri wa hazina, Janet Yellen na Balozi wa Marekani Linda Thomas-Greenfield waliotembelea mwezi Januari kuzungumzia juu ya kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Afrika.

XS
SM
MD
LG