Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:42

Jill Biden ahimiza vijana wa Namibia kutetea demokrasia akielekea Kenya


Mke wa rais wa Namibia, Monica Geingos, akiwa pamoja na mke wa rais wa Marekani Jill Biden katika ikulu ya rais ya Windhoek, Namibia, Feb. 23, 2023.
Mke wa rais wa Namibia, Monica Geingos, akiwa pamoja na mke wa rais wa Marekani Jill Biden katika ikulu ya rais ya Windhoek, Namibia, Feb. 23, 2023.

Mke wa raia wa Marekani Joe Biden, Dr. Jill Biden, ameambia vijana nchini Namibia kupigania na kulinda demokrasia ambayo wazazi na babu wao walipigania.

Jill Biden amehimiza wasichana na akina mama nchini Namibia kujihusisha zaidi na kukuza demokrasia nchini mwao.

Alikuwa akihutubua wanafunzi katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Namibia.

Amesisitiza kwamba ukujazi wa demokrasia hauna mwisho.

Namibia ni nchi changa katika demokrasia, baada ya kupata uhuru kutoka kwa Afrika kusini mwaka 1990.

Jill Biden amewasili Nairobi leo alasiri saa za Afrika mashariki.

Ziara yake Afrika inaangazia namna ya kuwawezesha wasichana na akina mama, pamoja na kuangazia ukosefu wa chakula kutokana na kiangazi ambacho kimeathiri pembe ya Afrika.

XS
SM
MD
LG