Mitandao ya kijamii inatakiwa itumike kama nyenzo katika mapambano ya kuzuia na kutokomeza ugonjwa wa UKIMWI ambao umewaathiri mamilioni ya watu barani Afrika.
Ziara ya mfalme Charles wa Uingereza imezua hisia tofauti miongoni mwa Wakenya, ambao baadhi yao wanaiona ziara hiyo kuwa fursa nzuri ya kuimarisha uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.
Kushuka kwa thamani ya sarafu ya Kenya kunamaanisha kuwa Wakenya wanatakiwa kufanya kazi zaidi na kuongeza kiwango na ubora wa uzalishaji katika soko la kimataifa.
Kumekuwa na maoni mchanganyiko miongoni mwa Wasudan kuhusiana na hatma ya mapigano yanayoendelea kati ya majenerali wawili waliohasimiana. Huku baadhi yao wakiwa na matumaini huenda mapigano yakamalizika na wengine wakiwa wamepoteza matumani ya kurejea kwa amani katika taifa hilo la Afrika.
Lugha za asili barani Afrika ni vyema zitumike katika kuboresha msamiati wa Kiswahili ili kuendelea kukikuza na kutumika katika nyanja mbali mbali ikiwemo katika fani za sayansi na teknolojia.
Tasnia ya habari nchini Tanzania inaomboleza kifo cha mwandishi wa habari mkongwe na mmoja wa waanzilishi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Leila Sheikh ambaye alifariki ghafla usiku wa kuamkia Jumatatu. Chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana.