Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 14:40

Ziara ya Mfalme Charles wa Uingerenza nchini Kenya yazua hisia tofauti


Mfalme Charles wa Uingereza na mkewe Malkia Camilla wakiwa kwenye balcony ya kasri ya Buckingham Mei 6, 2023. Picha na Oli SCARFF / AFP.
Mfalme Charles wa Uingereza na mkewe Malkia Camilla wakiwa kwenye balcony ya kasri ya Buckingham Mei 6, 2023. Picha na Oli SCARFF / AFP.

Ziara ya mfalme Charles wa Uingereza imezua hisia tofauti miongoni mwa Wakenya, ambao baadhi yao wanaiona ziara hiyo kuwa fursa nzuri ya kuimarisha uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

Huku baadhi ya Wakenya wakijiandaa kufanya maandamano kudai fidia kutokana na dhuluma zilizofanywa na wanajeshi wa Uingereza katika kambi ya jeshi ya Nanyuki.

Wakinzungumza na Sauti ya Amerika, baadhi yao wamesema Kenya kutembelewa na mgeni huyo mwenye wadhifa wa juu, ni muafaka kabisa katika kukuza uhusiano na kuzifanya changamoto za nchi hiyo kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na migogoro ya kiuchumi na ya kisiasa kujulikana katika jumuiya ya kimataifa.

“Ujio wa mfame wa Uingereza ni wa kuimarisha uhusiano mzuri wa muda mrefu kati ya Uingereza na Kenya” alisema mhadhiri katika kitengo cha Elimu kwenye Chuo Kikuu cha Tom Mboya kilichopo Homabay, kaskazini mwa ziwa Victoria na kuongeza kuwa “kilichobaki ni jinsi gani Kenya itakavyochukulia uhusiano katika kufungua milango ya uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali kuanzia uchumi, utalii mpaka elimu”

Mfamle Charles wa Uingereza na mkewe Camila wakiwa na wenyeji wao Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na mkewe Salma, walipowasili Tanzania mwaka 2011. Picha na AFP PHOTO/STRINGER.
Mfamle Charles wa Uingereza na mkewe Camila wakiwa na wenyeji wao Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na mkewe Salma, walipowasili Tanzania mwaka 2011. Picha na AFP PHOTO/STRINGER.

Lakini baadhi ya Wakenya wamesema watafanya maandamano siku ya Jumanne kupinga ukatili waliofanywa na baadhi ya wanajeshi katika kambi ya Nanyuki pamoja na kuulalamikia utawala wa kikoloni.

Mfalme Charles anaanza ziara yake ya kwanza kama mfalme katika taifa la Jumuiya ya Madola, ambapo maoni yoyote atakayotoa juu ya historia ya ukoloni wa Uingereza yatafuatiliwa kwa karibu.

Charles anatarajiwa kukabiliana na "masuala yenye maumivu makubwa" ya uhusiano wa kihistoria wa Uingereza na Kenya -- yaani kipindi cha utawala wa Uingereza, ambao ulimalizika mwaka 1963, Kasri ya Buckingham imesema.

Hii itajumuisha "Dharura" ya 1952-1960, wakati mamlaka ya kikoloni ilitangaza hali ya dharura ili kukabiliana na kampeni ya msituni ya Mau Mau dhidi ya walowezi kutoka Ulaya .

Mfalme wa Uingereza atalitembelea jiji la Nairobi pamoja na mji wa bandari wa Mombasa , lakini siyo mji wa Nanyuki ambako kuna kituo cha mafunzo ya jeshi la Uingereza nchini Kenya (BATUK).

Forum

XS
SM
MD
LG