Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:19

Mfalme Mumbere alakiwa na umati mkubwa wa watu Uganda


Mji wa Kasese, anakoishi mfalme Charles Wesley Mumbere wa
falme ya Rwenzururu huko Magharibi mwa Uganda. Picha na REUTERS/James Akena
Mji wa Kasese, anakoishi mfalme Charles Wesley Mumbere wa falme ya Rwenzururu huko Magharibi mwa Uganda. Picha na REUTERS/James Akena

Mfalme wa kikabila wa Uganda alirejea nyumbani na kukaribishwa kishujaa siku ya Jumatano, baada ya waendesha mashtaka kufuta mashtaka dhidi yake yaliyokuwa yakimhusisha na mapigano makali yaliyosababisha mauaji ya watu wengi miaka saba iliyopita.

Umati wa watu wenye furaha ulitanda katika mitaa iliyopo Kusini-Magharibi mwa mji wa Kasese kumlaki Mfalme wa Rwenzururu Charles Wesley Mumbere, Baadhi yao wakipuliza filimbi na kucheza huku waendesha pikipiki wakipiga honi zao.

Shirika la utangazaji la serikali UBC lilichapisha picha za video za Mumbere, akiwa amevalia suti nyeusi, akipunga mkono kutoka kwenye gari na kuelekea kwenye umati mkubwa wa wafuasi.

Mumbere alikuwa akikabiliwa na msururu wa mashtaka yakiwemo ya uhaini, mauaji na ugaidi baada yake na dazerni ya watu wengine, walikamatwa mwezi Novemba mwaka 2016 wakati wa msako mkali wa polisi dhidi ya ikulu yake.

Mumbere, mfalme wa jadi wa ufalme wa Rwenzururu ulioko Magharibi mwa Uganda, alishutumiwa kwa kuwaamuru wanamgambo wa kasri yake kuunda taifa huru katika eneo linalozunguka Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Serikali ya Uganda ilisema zaidi ya watu 100 waliuawa katika mapigano ya siku mbili lakini mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema idadi ya waliouawa ni kubwa zaidi.

Mumbere aliwekwa gerezani kwa miezi kadhaa kabla ya kuachiliwa kwa kifungo cha nyumbani katika mji wa Kampala, ambako alikaa hadi mapema mwaka huu.

Waendesha mashtaka walifuta kesi hiyo mwezi Juni dhidi ya mfalme huyo na watumuhiwa wengine zaidi ya 200 walioshtakiwa pamoja naye, lakini mfalme huyo hadi sasa amezuiliwa kurejea katika ufalme.

Ufalme wa Rwenzururu wa watu wa kabila la Bakonzo una historia ya mielekeo ya kutaka kujitenga na mivutano ya muda mrefu na serikali ya Uganda.

Baada ya kunyakua mamlaka mwaka 1986, Rais wa muda mrefu Yoweri Museveni alirejesha falme kadhaa za jadi ikiwa ni pamoja na Rwenzururu ambayo ilitambuliwa rasmi na serikali mwaka 2009.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG