Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 04:44

ICC yaripoti tukio la udukuzi dhidi ya mtandao wake


Makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu (ICC), mjini The Hague Uholanzi
Makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu (ICC), mjini The Hague Uholanzi

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) Jumanne imefichua kisa cha udukuzi, tukio la kihalifu katika moja ya taasisi zenye hadhi ya juu duniani.

ICC imesema iligundua shughuli isiyo ya kawaida kwenye mtandao wa kompyuta zake mwishoni mwa wiki iliyopita, na inaendelea kushughulikia tatizo hilo.

Msemaji wa mahakama hiyo amekataa kutoa maelezo juu ya ukubwa wa udukuzi huo, na iwapo tatizo hilo limemalizika kabisa au nani alifanya udukuzi huo.

“Hatua za haraka zilichukuliwa kukabiliana na tukio hilo la udukuzi wa mtandaoni na kupunguza athari zake,” ICC imesema katika taarifa.

Mahakama hiyo ya uhalifu wa kivita yenye makao yake the Hague Uholanzi, iliundwa mwaka 2002 kushughulikia kesi za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Waendesha mashtaka kwenye mahakama hiyo kwa sasa wanafanya uchunguzi wa kesi 17 kuhusu Ukraine, Uganda, Venezuela, Aghanistan na Ufilipino kati ya nyingine.

Forum

XS
SM
MD
LG