Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 14:23
VOA Direct Packages

Wamaasai kumuomba Mfalme Charles III atakaye zuru Kenya awasaidie kurejeshewa ardhi yao


Mwenyekiti wa kundi la wazee wa jamii ya  Wamaasai, Mzee Kelena Olenchoy akiwa na viongozi wenzake.
Mwenyekiti wa kundi la wazee wa jamii ya  Wamaasai, Mzee Kelena Olenchoy akiwa na viongozi wenzake.

Nchini Kenya, siku Tatu Kabla ya Mfalme wa Uingereza Charles III kuzuru taifa hilo  kundi la wazee wa jamii ya  Wamaasai sasa wanadai  kurejeshewa ardhi wanayodai walipokonywa wakati wa vita vya kujinyakulia uhuru taifa hilo.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Mzee Kelena Olenchoy, wazee hao wanadai ardhi ya takriban ekari milioni 700 waliyopokonywa wakati wa vita vya kudai uhuru.

Ardhi hiyo inatumiwa na Waingereza kuendeleza shughuli za biashara ikiwemo mbuga za wanyama binafsi na ukulima kwa sasa.

“Ipo baadhi ya miji ambayo japo ilikuwa yetu wanaoishi hapo ni Wakenya, hiyo hatutaki kurejeshewa ila tulipwe fidia. Lakini ardhi inayotumiwa na Waingereza kwa sasa kufuga wanyama turudishiwe pamoja na hao wanyama maana ni wetu,” mzee Olenchoy.

Mzee Olenchoy anasema wanadai fidia kutokana na madhila waliyopitia wakati wa vita hivyo na pia msamaha wa hadharani kutoka kwa Mfalme wa Uingereza Charles III.

Wazee hao ambao pia wametuma maombi la kutaka kufanya mazungumzo na Mfalme Charles wakati wa ziara yake nchini Kenya aidha wametishia kuelekea mahakamani kudai haki yao.

Mfalme Charles III na Malkia Camilla wanatarajiwa kuzuru Kenya kati ya tarehe 31 mwezi Oktoba na taehe 3 mwezi Novemba, hii ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika mataifa ya jumuiya wa madola tangu kutawazwa kuwa Mfalme.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Zainab Said, Kenya.

Forum

XS
SM
MD
LG