Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:51

Mjane wa mwanahabari wa Pakistan aliyeuwawa Nairobi afungua mashitaka dhidi ya polisi wa Kenya


Mwanahabari wa Pakistan Arshad Sharif aliyeuwawa mjini Nairobi 2022.
Mwanahabari wa Pakistan Arshad Sharif aliyeuwawa mjini Nairobi 2022.

Mjane wa mwandishi wa habari wa Pakistan aliyeuawa  na polisi wa Kenya baada ya kukimbia  kukamatwa nchini mwake, leo amefungua mashtaka dhidi ya Idara ya polisi ya Kenya, wakili wake amesema.

Arshrad Sharif aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa kijeshi wa Pakistan, na mfuasi sugu wa waziri mkuu wa zamani, Imran Khan, alikufa baada ya kumiminiwa risasi kwenye kizuizi cha polisi nje ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi mwaka uliopita.

Javeria Siddique ambaye ni mmoja wa wake wawili wa Sharif, wiki iliyopita aliliambia shirika la habari la AFP akiwa mjini Islamabad kwamba angefungua mashitaka hayo.

Wakili wake Ochiel Dudley amethibitisha kwamba mashitaka hayo yamewasilishwa mapema leo mbele kwenye mahakama kuu ya Kenya mwaka mmoja tangu kutokea kwa kifo hicho.

Amesema kwamba wanachosubiri sasa ni maelekezo zaidi kutoka kwenye mahakama.

Forum

XS
SM
MD
LG