Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:40

Kuanguka kwa bei ya kahawa na ukame kumewayumbisha wakulima wa Uganda


Mkulima akivuna kahawa huko Bali, Indonesia. Gharama za  usafirishaji kwa kontena lenye futi 20 linalosafirishwa kutoka Indonesia hadi Amerika Kaskazini, kwa mfano, linakadiriwa kugharimu dola 800 -1000 hivi sasa.
Mkulima akivuna kahawa huko Bali, Indonesia. Gharama za  usafirishaji kwa kontena lenye futi 20 linalosafirishwa kutoka Indonesia hadi Amerika Kaskazini, kwa mfano, linakadiriwa kugharimu dola 800 -1000 hivi sasa.

Bei ya kahawa na gharama za usafirishaji kimataifa zimeshuka katika robo ya mwisho ya mwaka 2022.

Sekta ya kahawa nchini Uganda inaelekea katika changamoto za 2023 zinazo elezewa na kushuka kwa bei na utabiri wa kupungua kwa uzalishaji kufuatia kipindi cha ukame kilichoathiri maeneo makuu yanayopanda kahawa.

Wakati sekta hiyo ilikuwa inashamiri kati ya 2020 na 2022 – huku bei ya kahawa ikipanda, kuongezeka kwa kiwango cha usafirishaji nje na mapato yakuridhisha kwa wakulima – kushuka kwa gharama za usafirishaji kimataifa na utabiri unaoonyesha kuongezeka uzalishaji nchini Brazil ulichochea kuanguka kwa bei ya kahawa katika robo ya mwisho ya 2022, kulingana na wafanyabiashara katika soko hilo.

Gharama za usafirishaji za kimataifa zilishuka kutoka rekodi ya juu ya dola 10,000 zilizotozwa kwa kontena katika baadhi ya njia za baharini mwezi Januari 2022 kufikia chini ya dola 2,000. Gharama za usafirishaji kwa kontena lenye futi 20 linalosafirishwa kutoka Indonesia hadi Amerika Kaskazini, kwa mfano, linakadiriwa kugharimu dola 800 -1000 hivi sasa.

Kwa sababu hiyo, bei ya kahawa katika eneo na kimataifa imeshuka tangu Oktoba 2022.

Bei ya kahawa aina ya robusta kimataifa imeporomoka kutoka wastani wa dola 2,400 kwa tani hadi dola 1,856 kwa tani kufikia mwisho wa mwaka jana, kulingana na takwimu za sekta hiyo.

Bei ya eneo ya kahawa ya robusta imeshuka kutoka Ush 7,200 ($1.9) kwa kilo hadi Ush 5,800 ($1.6) kwa kilo katika kipindi cha nusu ya pili ya mwaka 2022 wakati kahawa aina ya Arabica bei yake ilianguka kutoka Ush 11,000 ($2.9) kwa kilo hadi Ush8,000 ($2) kwa kilo katika kipindi hicho.

Uzalishaji wa Kahawa ya Robusta unachangia kwa zaidi ya asilimia 60 ya kilimo cha kahawa kwa ujumla nchini Uganda.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa nchini Kenya.

XS
SM
MD
LG