Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:52

Muhoozi Kainerugaba anataka kushindana na baba yake, Yoweri Museveni kuongoza Uganda?


Rais wa Uganda Yoweri Museveni Feb 11, 2020
Rais wa Uganda Yoweri Museveni Feb 11, 2020

Mawaziri nchini Uganda wameendelea kumkosoa mtoto wa rais Yoweri Museveni baada ya kuonyesha dalili za kutaka kugombea urais na badala yake wameanza kampeni ya kuhakikisha kwamba Museveni anagombea mhula mwingine madatakani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2026.

Museveni mwenye umri wa miaka 78, ametawala Uganda kwa muda wa miaka 37, tangu mwaka 1986 hajasema iwapo atagombea mhula mwingine lakini kuna shinkizo kutoka kwa mawaziri wake kwamba watahakikisha anaendelea kutawala.

Mtoto wa Museveni Generali Muhoozi Kainerugaba, mwenye umri wa miaka 48, anapigiwa kampeni na wafuasi wake kuwania urais.

Muhoozi amekuwa akikosoa sana chama kinachotawala cha National resistance Movement NRM, kinachoongozwa na babake, rais Yoweri Museveni.

Naibu wa rais wa Uganda Jessica Alupo, ni wa hivi punde kusema kwamba rais Museveni atagombea mhula mwingine madarakani katika uchaguzi wa mwaka 2026.

Alupo, ambaye ni mwanajeshi mstaafu, amesema kwamba Museveni ameiweka Uganda kwenye mazingira mazuri sana ya maendeleo na kwamba ndiye mwenye uwezo wa kuleta maendeleo nchini humo.

“Museveni atakuwa na sisi mwaka 2026. Kwa hivyo, nawaomba muendelee kumuunga mkono namna ambavyo mumekuwa mkifanya,” amesema makam rais Jessica Alupo.

https://www.voaswahili.com/a/siasa-za-kumrithi-museveni-majenerali-wastaafu-wajibizana-na-muhoozi-kainerugaba/6907545.html

Nia ya Generali Muhoozi kugombea urais

Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museveni
Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museveni

Matamshi ya Alupo yanajiri siku chache baada ya waziri wa mambo ya ndani Meja Jenerali Kahinda Otaffire kujibizana na Muhoozi Kainerugaba kuhusu nia yake ya kugombea urais nchini Uganda.

Muhoozi ambaye anajiita kuwa ‘standby generator’ yani nguvu za umeme mbadala, maana yake kwamba yupo tayari kuchukua uongozi wa Uganda wakati wowote babake anaondoka, amesema kwamba wakati wa viongozi wa sasa walio madarakani imemalizika na ni wakati wa kizazi cha Muhoozi.

Otafiire, badala yake amesema kwamba Muhoozi ni ‘generator’ iliyokufa, na kwamba kama anataka kujihusisha na siasa, astaafu kutoka jeshi kwanza.

Muhoozi ametaka vigogo wa chama cha NRM kuwa watu wasio na fikra na mipango kwa nchi na ambao fikra zao ni za kufanya mambo kwa kushitukia tu, pale yanapotokea bila mpangilio.

Muhoozi amekuwa akisema kwamba yeye ndiye aliye na suluhisho kwa matatizo ya Uganda.

XS
SM
MD
LG