Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 16:57

Uganda imevunja mpango wake na China kuhusu ujenzi wa SGR


Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiwa na rais wa China Xi Jinping katika mojawapo ya hafla mjini Beijing, China, March 31, 2015.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiwa na rais wa China Xi Jinping katika mojawapo ya hafla mjini Beijing, China, March 31, 2015.

Serikali ya Uganda imevunja mkataba na kampuni ya China ya Harbour Engineering (CHEC) kujenga awamu ya kwanza ya reli yenye umbali wa kilomenta 273 kutoka Malaba hadi Kampala.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na gazeti la The East African, Mkataba huo umevunjwa baada ya miaka nane ya kukosa utekelezaji.

Njia hiyo ya reli, inaanzia Malaba, kwenye mpaka wa Uganda na Kenya, ilitarajiwa kugharimu dola za kimarekani billion 2.2, lakini wafadhili kutoka China wameshindwa kuufadhili mradi huo baada ya kuitilia shaka SGR upande wa Kenya, kufika kwenye mpaka ili kuungana na Uganda na kuifanya mradi uwe wa mafanikio.

Mratibu wa mradi SGR, Injinia Perez Wamburu amesema, Kampala imesaini makubaliano (MOU) na kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi. Kampuni hiyo inatarajiwa kuwasilisha majibu ya mapendekezo ya serikali kuhusiana na ujenzi huo ndani ya wiki chache zijazo, ikifungua njia kwa ununuzi.

Kampala imesema ufadhili wa mradi huo pia utabadilika , Yapi Merkezi, ambayo inajenga reli ya Tanzania, inatarajiwa kushirikiana na mashirika yake ya utoaji wa mikopo (ECA) ili kufufua mradi huo.

Gazeti la The East Africa limeona mapendekezo kati ya serikali ya Uganda na wafadhili wanaotarajiwa kuufadhili mradi huo ikiwemo UK Export Fund, (UKEF) ambao Septemba mwaka jana ilihusishwa katika mjadala wa ufadhili wa ujenzi wa reli hiyo kwa gharama kati ya paundi 1.5 billion au $1.72 billion.

Kushindwa kwa benki ya Exim ya China kuendeleza mradi huo, Rais Yoweri Museveni mwaka jana aliwaelekeza maafisa wake watafute wafadhili kutoka taasisi nyingine za fedha duniani, London na UKEF zilikuwa taasisi za mwanzo kuwasiliana nao Septemba mwaka jana, Chanzo cha habari kilicho karibu na mradi huo kimeeleza.

Wambura amesema, Mwanasheria mkuu wa Uganda Kiryowa Kiwanuka kwa haraka aliupitia mkataba wa CHEC mara baada ya kuonekana kuwa Exim ya China --- Mfadhili wa mradi mkubwa wa miundo mbinu wa Kampala, kwa muda wa miaka kumi – imeshindwa kutoa ufadhili wa mradi huo.

XS
SM
MD
LG