Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:31

Mahakama nchini Uganda yafuta kifungu cha sheria inayotumika dhidi wa wakosoaji wa Museveni


Msomi Stella Nyanzi alipokuwa anakamatwa na maafisa wa polisi kwa sababu ya alikuwa anakosoa namna serikali ilivyokuwa inagawa chakula cha msaada na kuweka amri ya kutotoka nje kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona nchini Kampala.
Msomi Stella Nyanzi alipokuwa anakamatwa na maafisa wa polisi kwa sababu ya alikuwa anakosoa namna serikali ilivyokuwa inagawa chakula cha msaada na kuweka amri ya kutotoka nje kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona nchini Kampala.

Mahakama nchini Uganda imefuta  kifungu cha sheria ya mawasiliano  ambacho kinatumika kuwashtaki wakosoaji wa serikali,  waandishi wa habari na waandishi wengine wakiwemo  wawili waliokimbilia nchini Ujerumani. 

Kwa mujibu wa sheria ya matumizi mabaya ya kompyuta, moja ya kifungu kinazuia matumizi ya mawasiliano ya kielektroniki “kuvuruga amani, utulivu au haki ya faragha ya mtu yeyote bila ya dhamiri ya mawasiliano halali.”

Adhabu kwa watuhumiwa inaanzia faini kubwa ya fedha taslimu mpaka kifungo cha jela cha miaka kadhaa.

Katika uamuzi kufuatia maombi yaliyowasilishwa na mwanaharakati wa haki akitaka kufutwa kwa kifungu hicho cha sheria, Mahakama ya Katiba ilikubaliana na ombi hilo, ikisema kuwa ilikuwa imekiuka katiba.

Jaji wa mahakama ya katiba Kenneth Kakuru ambaye aliandika hukumu hiyo kwa niaba ya jopo la majaji watano, amesema kwamba kifungu hicho cha sheria “ si halali na kinakandamiza uhuru wa kuzungumza katika jamii huru na ya kidemokrasia ”

Ametangaza kuwa kipengele hicho cha sheria “ni batili” na kusitisha utekelezaji wake.

Shirika la habari la Reuters limefanya jitihada za kumpata msemaji wa serikali Ofwono Opondo, lakini limeshindwa kupata majibu ya haraka .

Wanaharakati wa haki wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kuhusu sheria kadhaa za mawasiliano zilizowekwa na serikali ya Yoweri Museveni.

Wakosoaji wamesema sheria hazichagui zinalenga yeyote, zinahila za kudhibiti habari na mara nyingi zimetumika kuwaadhibu wapinzani wa Museveni ambaye amekuwa akiiongoza Uganda tangu mwaka 1986.

Stella Nyanzi, ni mhadhiri na mwandishi ambaye amepata umaarufu katika mitandao ya kijamii kutokana mashambulizi yake ya matusi na kashfa dhidi ya Museveni, alifungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka sheria hiyo ya Uganda ya mawasiliano ya kielektroniki.

Baadaye aliikimbia Uganda, na kuomba hifadhi nchini Ujerumani ambako anaishi mpaka sasa akiwa na mwandishi mwingine ambaye ni mshindi wa tuzo ya kimataifa, Kakwenza Rukirabashaija ambaye pia alihukumiwa chini ya sheria hiyo kabla ya kukimbia nchini.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa Kenya

XS
SM
MD
LG