Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:52

Polisi wa Uganda wakamata zaidi ya wafuasi 30 wa upinzani


Kiongozi wa upinzania wa Uganda Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Kyagulanyi Ssentamu, alipozungumza na AP.
Kiongozi wa upinzania wa Uganda Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Kyagulanyi Ssentamu, alipozungumza na AP.

Polisi nchini Uganda wametumia  gesi ya kutoa machozi na kuwakamata zaidi ya wafuasi 30 wa upinzani baada ya kuhudhuria mkutano wa sala ulioandaliwa na mwanamuziki ambaye amekuwa mwanasiasa Bobi Wine.

Polisi wanasema mkutano huyo ulikuwa kinyume cha sheria kwa viel waandaaji walishindwa kumjulisha mkuu wa polisi kabla ya kuitisha mkutano huo.

Polisi wa Uganda wamethibitisha kuwakamata takriban wanachama 30 wa chama cha upinzani cha Bobi Wine, wakati wa mkutano was ala ulioandaliwa na kundi mwamvuli la chama hicho, United Forces of Change.

wale waliokusanyika walipanga kufanya ibada kwa ajili ya watu waliokamatwa, waliofariki, waliotekwa na wafuasi wote wa upinzani, hasa kutoka chama cha wine cha National Unity Platform, ambao hawajulikani walipo katika muda wa miaka mwili iliyopita.

wanachama wengine wa upinzani ni pamoja na Conservative Party na Forum for Democratic Changes.

Lakini, Lucas Owoyesigyire, naibu msemaji wa Polisi jijini Kampala, ameiambia VOA kwa njia ya simu, kwamba kundi la upizani halikumpa Inspekta Jenerali wa Polisi, Okoth Ochola taarifa ya mapema kuhusu mkutano huo wa salam ili awezi kuweka ulinzi unaohitajika – kutokana na vitisho vinavyoendelea vya ugaidi.

Bwana Owoyesigyire anasema “sehemu hii ilikuwa ya umma. Walitakiwa kumjulisha IGP, hasa wamiliki wa eneo hilo, wangemueleza IGP kuhusu hili. Kwahiyo, hatukuwea kuwaruhusu waendelee na mipango yao. ndiyo, tuna baadhi wa washukiwa hapa, katika kituo kikuu cha polisi CPS lakini ni zaidi ya 30.”

Mwanasiasa wa Uganda, Joel Ssenyonyi, ameiambia VOA kwamba walililpia eneo hilo lakini walipowasili Ijumaa asubuhi, polisi na jeshi walikuwa wamelizingira na kuwalazimisha wasali nje.

“Kwa kweli, tulipofika huko, tuliona mmoja wa watu ambaye alikuwa na watu wengi. Tulimuomba, tafadhali njoo uzungumze na sisi, alikataa kuja, kwasababu sisi tulikuwa mlangoni, hawakuturuhusu kuingia ndani. Sheria inasema tutoe taarifa….sheria haisemi tuombe ruhusua. Tuliwajulisha na kuwaomba watupatie ulinzi kwa ajili ya shughuli yetu iendelee bila ya tatizo. Kwasababu tutakuwa ndani ya jengo,” amesema Ssenyonyi.

Katika muda wa miaka miwili iliyopita, hasa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2021, idadi ya wafuasi wa upinzani waliingizwa katika magari na kuchukuliwa sehemu zinazojulikana na zisizojulikana na kuwekwa ndani.

Wakati wengi walirejea wakiwa wamekatwa viungo, kudai kuteswa, wengi wao wanashukiwa ama wamefariki au bado wako kizuizini. Upinzani unasema umetoa majina yao mara kadhaa kwenye bunge, na kwenye bunge na kuelezewa wanashikiliwa na usalama na kudai maelezo kutoka serikalini bila ya maelezo yoyote .

mpaka hivi leo, utekaji unaendelea, ikiwemo Kirumira Marvin Godfrey mwenue umri wa miaka 17, ambaye alikamatwa kutoka kwenye sehemu anakofanyia kazi ya kumenya viazi.

akiongea na VOA, mama yake Godfrey, Nambazira Sauda, anakumbula kwamba Novemba 5, rafiki wa mtoto wake wa kiume alimueleza kuhusu kupotea kwa mwanawe. Tangu wakati huo, Sauda anasema amejaribu kumtafuta katika kila vituo ambacho watu wanazuiliwa bila ya mafanikio, na khofu aliyonayo ni kwamba mtoto wake amekufa.

Anasema, “wanasema mtoto anapofariki, mama anapata maumivu ya uchungu wa kujifungua. Nilikwenda bafuni wakati wote, siwezi kula, siwezi kunywa, nilipoteza hisia zangu.”

anasema “ninapoanza kutembelea, najikuta natembea kutoka sehemu moja hadi nyingi. Kwasababu mtoto wangu ni mdogo. Ni bora waje waniue mimi badala yake, analia kila siku.”

Rais Yoweri Museveni katika miezi ya karibuni alielezea kuwa hafahamu kuhusu utekaji wowote unaoendelea nchini kwake. Pia alisisitiza kwamba makosa yoyote yanayofanywa na wana usalama wakati wakiwa kazi yanarekebishwa.

bado haiko bayan ani wanachama wangapi wa kundi la upinzani ama wamekufa au wako kizuizini.

XS
SM
MD
LG