Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:08

Kenya yatoa onyo la kidiplomasia kwa Ethiopia


Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed (L) na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta Kaunti ya Lamu, Kenya Disemba 9, 2020. Presidential Press Service/Handout via REUTERS
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed (L) na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta Kaunti ya Lamu, Kenya Disemba 9, 2020. Presidential Press Service/Handout via REUTERS

Katika taarifa kwa balozi za  kigeni na ofisi za mashirika za kimataifa zilizoko  Nairobi wizara ya mambo ya nje ilisema itaruhusu upitishaji wowote wa wafanyakazi au vifaa kutoka nchi ya tatu kupitia Kenya lakini kama  tu wanakidhi vigezo pamoja na idhini za awali

Kenya inasema itazuia harakati zozote za upelekaji jeshi au kidiplomasia kupitia eneo lake baada ya kuhamishwa kwa muda kwa wafanyakazi wa kigeni kutoka Ethiopia kwa sababu za usalama kulingana na gazeti la Daily Nation.

Katika taarifa kwa balozi za kigeni na ofisi za mashirika za kimataifa zilizoko Nairobi wizara ya mambo ya nje ilisema itaruhusu upitishaji wowote wa wafanyakazi au vifaa kutoka nchi ya tatu kupitia Kenya lakini kama tu wanakidhi vigezo pamoja na idhini za awali.

Maelezo hayo yanayojulikana kama “maelezo ya maneno” katika misingi ya kidiplomasia hayaitaji Ethiopia kwa jina lakini inasema matukio ya hivi karibuni katika eneo hilo yanaweza kuzilazimisha baadhi ya nchi za kigeni kuhamishia jeshi na waanyakazi wa kidiplomasia kwenda Kenya na lazima itifaki ifuatwe katika kufanya hivyo.

XS
SM
MD
LG