Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:06

Raila Odinga anatangaza azma yake kuwania urais Kenya kwa mara ya tano


Kiongozi wa upinzani Kenya, Raila Odinga akiwa Nairobi, Kenya, Feb. 1, 2018.
Kiongozi wa upinzani Kenya, Raila Odinga akiwa Nairobi, Kenya, Feb. 1, 2018.

Mara tatu za mwisho za Odinga kuwania nafasi hiyo ni mwaka 2007, 2013 na 2017 ambapo kulikumbwa na mvutano pamoja na ghasa zilizosababishwa na wafuasi wake kwa kuandamana, kupinga matokeo au kuipa changamoto mahakama, wakisema aliibiwa ushindi

Kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, leo Ijumaa ametangaza kwa mara ya tano azma yake ya kuwania urais, safari hii akiungwa mkono na aliyekuwa adui yake, Rais Uhuru Kenyatta.

Wapiga kura katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi Afrika mashariki wanatarajiwa kupiga kura Agosti 2022 lakini jina la Kenyatta halitakuwa kwenye sanduku la kura kutokana na kikomo cha mihula kwenye katiba cha kuhudumu mihula miwili ya miaka mitano kila moja.

Mara tatu za mwisho za Odinga kuwania nafasi hiyo ni mwaka 2007, 2013 na 2017 ambapo kulikumbwa na mvutano pamoja na ghasa zilizosababishwa na wafuasi wake kwa kuandamana, kupinga matokeo au kuipa changamoto mahakama, wakisema aliibiwa ushindi.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (L) na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, Machi 9, 2018. (Facebook/Uhuru Kenyatta)
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (L) na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, Machi 9, 2018. (Facebook/Uhuru Kenyatta)

Mapigano yaliyosababisha vifo yalitokea katika kura za mwaka 2007 na 2017. Lakini Raila alikutana na Kenyatta na kuleta mazingira ya amani mwanzoni mwa mwaka 2018 na kumuweka kando naibu wa Kenyatta, William Ruto ambaye amekuwa akiongea kuhusu azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa kenya hapo mwakani.

XS
SM
MD
LG