Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:40

Gharama ya masomo ni ghali sana Afrika - UNESCO


Wanafunzi wakiwa darasani mjini Kinshasa, DRC
Wanafunzi wakiwa darasani mjini Kinshasa, DRC

Ripoti ya idhara ya elimu katika umoja wa mataifa - UNESCO, inasema kwamba familia katika nchi zilizo jangwa la Sahara zinatumia kiwango kikubwa cha mapato yao kulipa karo ya watoto shuleni, huku wengi wao wakikosa kupata elimu ya kiwango bora.

Kwa jumla, karibu asilimia 40 ya pesa karo inalipwa na familia na wala sio serikali.

Ripoti ya Unesco iliyotolewa leo Ijumaa, na inayoangazia hali ya elimu kote duniani, inasema kwamba kuna hatari inayokuja ya kutokuwepo kiwango cha elimu sawa, sawa na namna elimu hiyo inavyotolewa kwa kuwatenga wengine.

Ripoti hiyo inaonya kwamba asilimia 8 ya familia katika nchi zenye mapato ya kiwango cha chini na zile zenye kiwango cha kati zinalazimika kukopa pesa ili kulipia waotot wao karo shuleni.

Kiwango cha karo ni cha juu katika nchi kama Uganda na Kenya ambapo theluthi tatu ya familia zinahitajika kuchukua mikopo ili kulipa karo.

Unesco inataka serikali kutoa elimu ya bure na ya kiwango cha juu kwa wanafunzi wote ili kuwanufaisha watoto kutoka familia maskini.

XS
SM
MD
LG