Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:09

Kenyatta anawahakikishia wakenya BBI ipo hai


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Akihutubia wananchi wakati wa sherehe za maadhimisho ya  miaka 57 ya Jamhuri Day kwenye bustani ya Uhuru jijini Nairobi Rais Uhuru Kenyatta alieleza kuwa ndoto ya BBI bado ipo katika jitihada za kuzungumzia  swali la mshindi anachukua vyote katika uchaguzi

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewahakikishia wakenya kwamba mipango ya kufanya marekebisho ya katiba ya mwaka 2010 kupitia “Building Bridges Initiative (BBI) ambayo yalikabiliwa na vikwazo vya kisheria yatatimizwa, kulingana na gazeti la Daily Nation.

Akihutubia wananchi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 57 ya Jamhuri Day kwenye bustani ya Uhuru jijini Nairobi, mkuu huyo wa nchi alieleza kuwa ndoto hiyo bado ipo katika jitihada za kuzungumzia swali la mshindi anachukua vyote katika uchaguzi. Ingawa ilikumbana na baadhi ya vikwazo vya kisheria, naweza kusema tu kwamba BBI ni ndoto iliyoahirishwa. Siku moja, itatokea, kwa sababu nchi haiwezi kustahmili ubaguzi wa kikabila na kutengwa kwa vile haiwezi kustahmili uwakilishi usio wa haki na potofu, Rais alisema.

Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Wakati huo huo Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa gharama ya umeme itapungua kwa angalau asilimia 15 kabla ya Krismas. Rais Kenyatta alisema kupunguzwa kwa gharama ya umeme kutatekelezwa kwa awamu mbili za asilimia 15 kila moja.

Alisema asilimia 15 ya kwanza, ambayo itafikiwa kupitia hatua za awali zinazozingatia mfumo na hasara ya kibiashara, zitaonekana kwenye bili za Disemba. Alisema kuwa punguzo zaidi la asilimia 15, litatekelezwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2022.

"Ninafuraha kuelezea kwamba njia za kupunguza gharama ya umeme kwa zaidi ya asilimia 30 iko katika mwelekeo" Rais Kenyatta alisema wakati alipoongoza sherehe za 57 za Jamhuri Day ambazo ni za mwisho kwa utawala wake, zilizofanyika kwenye bustani ya uhuru jijini Nairobi leo Jumapili.

XS
SM
MD
LG